Meneja Bidhaa za Intanet wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Abdul Mombokaleo akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya inayotoa fursa kwa mteja kufurahia huduma ya intaneti
na kujipatia modem ya bure. Kulia ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Laibu Leonard. (Picha na Francis Dande)
Meneja Bidhaa za Intanet wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Abdul Mombokaleoakionyesha vipeperushi vyenye maelekezo kuhusu promosheni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Laibu Leonard na Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashaki.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL),
imezindua promosheni mpya inayotoa fursa kwa mteja kufurahia huduma ya intaneti
na kujipatia modem ya bure.
Hayo yalisemwa na Meneja wa wa Bidhaa za
Intaneti, Abdul Mambokaleo, wakati alipozungumza na wandishi wa habari kuhusu
promosheni hiyo, jijini Dar es Salaam.
“Promosheni hii, ya ‘Dili la Ukweli’ ni
muendelezo wa kampuni yetu katika kuwapatia wateja wetu kile wanachokihitaji
wapatiwe,”alisema Mambokaleo.
Alisema, promosheni hiyo inatoa fursa
kwa wateja kufurahia modem ya bure pamoja na vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei
kwa kiwango ambacho kitamfanya Mtanzania wa kawaida aweze kutumia humuduma
hiyo.
“Kupata modem ya bure mteja atapaswa
kununua intaneti bila kikomo kw ash 20,000 ambayo itatumika ndani ya mwezi
mzima.
“Huduma hii ni kwa wateja wapya tu, kwa
mteja mwenye modem tumempa fursa ya kuchagua vifurushi ambavyo vimepunguzwa
bei,”alisema Mambokaleo.
Mambokaleo alisema promosheni hiyo ya
Dili la Ukweli inatoa fursa kwa mteja kufurahia punguzo la bei ya vifurushi vya
intaneti vya siku, wiki na mwezi kwa bei nafuu, kwa taarifa zaidi kila mteja
anaweza kutembelea ofisi zao.
No comments:
Post a Comment