Wazazi wa watoto waliozaliwa katika mkesha wa
Sikukuu ya Krismasi katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam jana,
wakiwa na afya nzuri pamoja na watoto wao. Kutoka kushoto ni Zamda Juma, Hadija
Shaibu na Maria Joseph. (Picha na Francis Dande)
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es
Salaam, Rashid Nyombiage akipima afya ya mtoto, Fredrick Mwita aliyezaliwa katika
mkesha wa Sikukuu ya Krismasi.
Na Mwandishi Wetu
WATOTO 71 wamezaliwa wakati
mkesha wa Krismasi katika Hospitali ya Amana na Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima
jijini, Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Amana Teresia Akida, alisema watoto waliozaliwa katika mkesha huo hospitalini hapo ni 52.wakiume ni 31 na wakike
21.
Akida alisema wazazi wa na
watoto hao wanaendelea vizuri huku akidai mzazi mmoja alijuifungua mapacha
watatu wakiume ambao siku zao zilikuwa hazijatimia.
Alisema changamoto kwa wazazi
katika hospital hiyo ni vifaa vya tiba vinakuwa vinapungua hali inayosababisha
kina mama kuagizwa baadhi ya vifaa vya kujifungulia.
“Mbali na changamoto hiyo pia
tunakabiliwa na upungudfu wa watendaji katika hospitali yetu hivyo tunaomba
serikali ilitupie jicho tatizo hilo”alisema.
Naye Muuguzi wa zamu
katika Hospitali ya Temeke, Rashidi
Nyombiage alisema watoto waliozaliwa katika mkesha huo hospitalin hapo ni
19 wakike tisa na wakiume 10.
Alisema waliozaliwa kwa njia
ya upasuaji ni wawili lakini hali zao zinaendelea vizuri pamoja na wazazi wao.
Alisema changamoto
inayokabili katika wodi za wazazi ni vitanda ni vichache havitoshelezi kwa kuwa
kila siku wazazi wanaongezeka hali inayosababvisha walale wawili hadi watatu
kwenye kitanda kimoja huku wengine wakilazimika kulala chini.
“Serikali ijaribu kutembelea
hospital kuona changamoto na kuweza kujua jinsi gani ya kuzitatua”Alisisitiza
Nyombiage.
Safi Mchala mkazi wa Tandika ambaye
alijifungua katika hospital hiyo, alisema amefurahi sana kujifungua mtoto wa
kike na kudai kuwa alikua anamuomba
mungu ampe mtoto wa kike hivyo anamshukuru mungu kumpatia mtoto aliyemuomba.
No comments:
Post a Comment