HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 13, 2015

Halmashauri ya Mufindi yapewa wiki 3 kujenga Kizimba cha takataka Soko Kuu Mafinga

Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu.
 vijana wa mafinga wakishangila uwepo wa Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu.

 Na Fredy Mgunda, mafindi.

Halmashauri ya mufindi yapewa wiki 3 kujenga kizimba cha takataka soko kuu mafinga pia kusambaza maji katika vyoo vya halmashauri vilivyopo sokoni hapo.

Wiki tatu hizo zimetolewa na Katibu wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi Miraji Mtatulu baada ya kufanya ziara ya kushtukiaza katika soko hilo na kubaini kuwapo kwa kizimba kinacho tumiwa kuhifadhi taka hakijajengwa kwa utalamu ikiwa kinauchafu na maji ya muvua nayo yanapita hapo hali inaypelekea kuhatalisha afya za wafanyabiashara katika eneo hilo hususani mlipuko wa magonjwa.

Pia mtatulu ametoa wiki tatu kwa halmashauri kukarabati miundo mbinu ya choo ambapo choo hiyo imekuwa ikitumiwa pasipo maji huku usafi wake nao ukiwa hafifu na kwaupande wa choo ya mtu binafsi ametakiwa kuweka maji vyooni na kuboresha usafi ndani ya wiki hizohizo tatu.

Nao wafanyabiashara wamemtaka kuchukua hatua stahiki kutokana na baadhi ya wataalamu wa serikali kuchukulia maneno ya wanasiasa ni siasa pia kutakiwa kuaahidi kama mambo hayo yasipofanyika ni hatua gani atachukua au nini afanyiwe,
"utatuaminisha vipi kuwa wewe utalifanyia kazi suala hili ikiwa hawa wataalamu wengi wao huamini maneno yanayozungumzwa na wanansiasa ni siasa" Akijibia amesema Ilikuonyesha amejitoa kufanya kazi ya jamii yeye hana tofauti na shehe,Mchungaji, au Padrii hivyo atahukumiwa siku ya mwisho hivyo hawezi acha ahukumiwa kwasababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji waliopewa jukumu la kufanya kazi hiyo.

Kwa upande wa katibu wa soko hilo FREDRICK MNG'ONG'O Ameibua changamoto ambayo kwasasa iliyokuwa mupango wa wafanyabiashara hao kujakugomea kitendo cha Serikali kupandisha kodi kwa asilimia mia huku TRA wakijipangia tuu kiasi cha kulipia kuwa ni mara 2 ya malipo ya mwaka jana jambo ambalo limewafanya wafanyabiasha wote kuitaka halmashauri kuandaa mkutano utakaotolea ufafanuzi juu ya swala hilo ikiwa na kuanika hadharani viwango vya ushuru kwa kila biashara ili kuondokana na rushwa za lazima huku wakimtaka na katibu huyokuhudhuria kutoa ushauriwake.

Mara baada ya kikao katibu amewataka wananchi kutokukichukia chama kilichopo madarakani kwani wanaokifanya chama hichohicho kutopendwa ni wafanyakazi wa sekta mbalimbali kutofanya kazi zao kwa maadili pia chama hicho hakiwatumi watumishi hao kuwaibia wananchi kwa maana ya kuwafisadi wananchi"Wananchi kwa pamoja tunatakiwa kuwawajibisha watendaji kwani wao ndio hawafanyikazi na chama kama chama kinafanya ipasavyo na sasa naanza na hawa ambao wao hawafanyi kazi za wananchi.

Katika kusisitiza na kujazia kuwa lazima baada ya wiki tatu anakagua tena kama yametendewa kazi amesema halmashauri inaweza kutumia fedha zitakazo ludishwa na waliozichukua kauli hiyo ilishangiliwa na wafanyabiashara waliokuwapo katika mkutano huo,kauli hiyo imekuja wakati baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri hiyo wakiwa wamefikishwa mahakama ya wilaya ya mufindi kwa makosa ya uhujumu uchumi katika halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages