Mwenyekiti wa Tamasha
la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es
salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi
ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.
Na Mwandishi Wetu
Aliongeza kuwa
ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu
ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema
maandalizi ya tamasha hilo
yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku
hiyo.
Alisema
wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni
waimbaji wa kimataifa Ephraim Sekeleti
wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu
wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili
nchini.
“Tamasha
la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama ishara ya kutakiana amani, upendo na mshikamano na tutaiombea nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu’’alisema Msama.
Msama
aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo
ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita
maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’
No comments:
Post a Comment