Na Bryceson Mathias
UNAODAIWA ni Ukatili wa
Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa Morogoro, umewakasirisha Wafanyakazi wa
Kiwanda hicho na kuwasababishia leo watinge bungeni Dodoma kwa Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, ili kumshitaki wakilalamikia Unyama wanaofanyiwa.
Wakionesha Sekula Na.C.1/18//2015 ya 22/3/2015 iliyonakiliwa
kwa Wakuu wa Idara wa Kapumpuni hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU) na Mbao za Matangazo kwa wafanyakazi wote,
wamedai ukatli huo hautekelezeki.
“Kutokana na Ukatili na Unyama aliotufanyia
mwekezaji kututaka tujaze fomu ya kufanya kazi kwa malipo ya kuchelewa kuanzia Mei
hadi Juni mwaka huu, na wasiotaka kujaza fomu hizo wajaze likizo bila malipo
ili wafanye shughuli zingine, ni kutufukuza kazi kienyeji".
“Hatua za kututaka tujaze fomu hizo kuanzia
26/03/2015 na kurudisha ofisini kabla ya 1/4/2015 saa mbili, na kwamba
mfanyakazi ambaye hatajaza kati ya fomu hizo kufanya kazi kwa malipo ya
kuchelewa au likizo bila malipo ndani ya siku tano atakuwa amejifukuzisha ni
ukatili” walisema wafanyakazi.
Kufuatia Tangazo hilo Maalum ambalo limesainiwa na
Kaimu Meneja Rasilimali, VT Mazengo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Mtibwa, Hamad
Yahaya, wafanyakazi hao wamekasirishwa na hawakuridhishwa nalo, na hivyo baada
ya Kikao wameamua Kutinga kwa Pinda bungeni.
Katika Msafara huo wa Watu Watano, wamo viongozi wa
Chama cha Wafanyakazi (TPAWU), Uongozi wa Wakulima Wadogo wa Miwa, Diwani wa Kata
ya Mtibwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Luka Mwakambaya.
Aidha mapema kabla ya hatua ya Wafanyakazi hao,
walipiga Kambi kwenye lango la mwekezaji kudai malipo na Mishahara ya mwezi wa 12. 2014 na Februai
2015, ambapo pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero kumtaka
Mwekezaji awalipe, hakutekeleza, hatua ambayo wafanyakazi na Wakulima wanaona
amefirisika, Serikali ipeleke mwekezaji Mpya.
No comments:
Post a Comment