Waendesha bodaboda na Bajaj mkoani Mbeya wakiwa katika mkutano wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na
Bajaji inayotolewa na Kampuniya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo
ilifanyika mjini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Dk.Charles Kimei akimkabidhi mwendesha bodaboda koti maalum kwa ajili ya usalama, Matokeo Swalo, mkazi wa mjini Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na Bajaji inayotolewa na Kampuniya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Nyerembe Munasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Dk.Charles (kushoto akimkabidhi kofia ngumu mwendesha bodaboda, Ponzi Manga mkazi wa mjini Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo ya Pikipiki na Bajaji inayotolewa na Kampuni ya CRDB Microfinance Services. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Nyerembe Munasa.
Na Esther Macha, Mbeya

MKURUGENZI
wa benki ya (CRDB) Dk. Charles Kimei amesema kuwa ili waendesha bodaboda waweze
kuwa na maisha mazuri hawana budi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ambazo
wanapata katika shughuli zao.
Amesema
kuwa ili kila mtu aweze kufanikiwa katika maisha ni vema kuweka akiba ambayo
nayo bila nidhamu ya matumizi huwezi kufika popote.
Dk. Kimei
amesema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya bodaboda
ambayo inaendeshwa na benki ya CRDB maarufu kwa jina la (Jiendeshe)
iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa uliopo jijini hapa.
Mkurugenzi
huyo aliwataka waendesha bodaboda kuweka akiba hata kama wanapata kidogo ikiwa
ni pamoja na kujiwekea malengo ya baadaye ili waweze kuwezesha shughuli zingine
ambazo zitawawezesha kufanya miradi mingine.
“Ndugu
zangu waendesha bodaboda mnapotumia fedha lazima mkumbuke kesho
,siyo unapata fedha unakimbilia kutumia katika masuala ya ulevi,mtu anayefanya
hivyo ujue hawezi kuwa tajiri kutokana na kuwa na matumizi mabaya ya fedha na
pamoja na kutojiwekea malengo”alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha
Dk. Kimei aliwataka waendesha bodaboda hao kama wanaona kuwa biashara hiyo
inakuwa na ushindani mkubwa ni vema wakabuni biashara nyingine ambayo inaweza
kuwa mbadala kwao.
“Najua
hivi sasa kwa uzinduzi huu wa huduma za mikopo ya boaboda biashara hii
itakuwa na ushindani mkubwa sana hivyo kama mkiona ushindani umekuwa mkubwa
jipangeni na kuanzisha miradi mingine ambayo itawawezesha kuendesha
maisha yenu”alisema.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa CRDB Microfinance benki,Sebastian
Masaki alisema kufunguliwa kwa wodi maalum kwa ajili waendesha bodaboda
si jambo zuri na kwamba asilimia 66 ya bajeti ya hospitali ya Mbeya huwa
inatengwa kwa ajili ya ajali za bodaboda.
Alisema
masuala ya ajali yasiwepo tena kwa waendesha bodaboda hivyo kikubwa waelimishwe
kuhusu ujasiriamali.
Naye
Katibu wa waendesha bodaboda Mkoani Mbeya Msumba Mbesa alisema kutokana na kuwa
na mazingira magumu ya biashara imewapelekea kufanya kazi mpaka usiku wa manane
ili waweze kufanikisha malengo ya fedha za matajiri wao.
Alisema
kwa hii mikopo ambayo Benki ya CRDB watakabidhi kwa waendesha bodaboda ambazo
watakuwa wanamiliki wenyewe zitaweza kusaidia waendesha bodaboda hao kumiliki za
kwao.
No comments:
Post a Comment