Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Ibrahim Issa wa kituo
cha Zaidia cha Sinza jijini Dar esSalaam wakati wa hafla ya kutoa zawadi za
Sikukuu ya Pasaka kwa vituo vya kulelea Watoto wanaoishi katika mazingita
magumu.
Watoto wakipokea zawadi za Sikukuu kuttoka kwa Msama.
Heid Edwin akiopkea zawadi za Pasaka kwa niaba ya watoto wezanke.
Charles Nyimbo akipokea zawadi za Sikukuu ya Pasaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions kwa niaba ya Kituo cha Malaika Kids cha Sinza.
Asante kwa zawadi za Sikukuumungu akubariki...
Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya watoto wakiwa na zawadi zao.
NA LOVENESS
BERNARD
Kampuni ya
Msama Promotions leo imetoa misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 7 vya kulelea
watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alex
Msama alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu ya mapato yatokanayo na Tamasha la
Pasaka.
‘’Misaada
hii ni mapato ya Tamasha la Pasaka mwaka jana
,tumewapa watoto zawadi hizi ili washiriki vema katika kusheherekea
sikukuu ya Pasaka na wajisikie kama watoto wengine’’, alisema Msama.
Kwa upande
wake mmoja wa walezi wa vituo hivyo Honoratha Michael ambaye ni mlezi wa kituo
cha Honoratha kilichopo Temeke, alisema kuwa anaishukuru Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwapa
misaada hiyo wanaomba nawatu wengine wajitolee kuwasaidia.
‘’Tunamshukuru
Msama na kampuni yake na hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea Baraka kutoka
kwa Mungu baba pia tunawaomba watanzania wengine wajitolee kwani tunazo
changamoto nyingi katika vituo vyetu’’alisema Honoratha.
Misaada hiyo
iliyotolewa jijini Dar es Salaam imegharimu million sita imewanufaisha
watotowa vituo vya Honoratha (Temeke),Malaika kids (Kinondoni),
Umra(Magomeni),Mwandaliwa( Boko), Zaidia (Sinza) na kituo cha Rahman kilichoko
Magomeni.
No comments:
Post a Comment