Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza leo. (Picha na Loveness Bernard)
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili
kutoka Uingereza leo.
Kutoka kushoto, Angela Kaonja, Nyakwesy Mujaya na Grace Khuni
Angela Kaonja akimvisha skafu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Nyakwesy Mujaya akimpa au mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi
Kelechi, akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions,
Nyakwesy Mujaya, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha
la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
Msama akipeana mkono na Ifeanyi
Kelechi,
Msama akiteta jambo na Ifeanyi
Kelechi,
Ifeanyi
Kelechi akiimba moja ya nyimbo zake.
Ifeanyi
Kelechi akiimba.
Miller Luwoye.
Anthonia Nwafor.
Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama (wa pili kulia) akiwa na waimbaji kutoka Uingereza.
NA LOVENESS BERNARD
MWIMBAJI wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini
Uingereza, Ifeanyi Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika
Tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili.
Kelechi, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), jana saa mbili asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar, akiongozana
na wenzake wanne.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Kelechi
alisema lengo la ujio wake ni kuhakikisha tamasha hilo linanoga kuliko
yaliyowahi kufanyika, ndio maana amekuja na jopo la waimbaji watano.
"Namshukuru Mungu kutufikisha salama, nimefurahi
sana kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, hasa kuja kuimba kwenye tamasha kubwa
kama hili, ambalo naamini litakuwa chachu ya kumfanya kila mtu kuvutiwa nalo,"
alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,
Alex Msama, alisema kuzidi kumiminika kwa waimbaji, kunaashiria tamasha hilo
litanoga zaidi.
"Waimbaji wetu wameshaanza kuwasili nchini na kesho
waliobakia watawasili...Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, tunaisubiria
siku hiyo tu,” alisema Msama.
Tayari muimbaji Faustine Munishi ‘Malebo’ mtanzania
anayeishi nchini Kenya tayari kawasili tangu juzi huku Ephraim Sekeleti wa
Zambia, Rebecca Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ kutoka Afrika Kusini
watafuata.
Mbali na waimbaji hao kutoka nje, watakuwepo pia wakali
wa hapa nchini wakiwamo Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro
na wengineo.
No comments:
Post a Comment