Askofu wa Kanisa
la Naioth Gospel ambaye pia ni Katibu Mkuu
wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka.
Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas hilo.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka. Kulia ni Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota.
NA LOVENESS
BERNARD
Askofu wa
Kanisa la Naioth Gospel Assembly, David
Mwasota amewataka wachungaji wote nchini
kuwaruhusu waumini wao kuhudhuria katika Tamasha la Pasaka
litakalofanyika April 5 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Askofu huyo amewataka wachungaji
wawaruhusu waumini waweze kusherehekea kufufuka kwake Yesu kristo kwa kusifu na kuabudu pamoja na waimbaji mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi.
Nawaomba
wachungaji wawaruhusu waumini baada ya ibada waje uwanja wa taifa tumsifu
muumba wa vyote kwa nyimbo na sala pamoja na waimbaji kutoka mataifa
mbalimbali.
Naye
Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama alisema waimbaji wameshaanza kuwasili
nchini wakiongozwa na Faustine Munishi (Malebo) ambaye aliwasili jana huku
Kerechi muimbaji kutoka Uingereza akitarajiwa kuwasili Jumamosi.
Maandalizi
tumekamilisha kwa asilimia 99 na waimbaji wameanza kuwasili nchini ambapo
Faustine Munishi mtanzania aishie nchini Kenya na kesho tunatarajia kumpokea
Ifeanyi Kerechi na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia huku Rebecca Malope na Solly
Mahlangu tukuwatarajia kuwasili Aprili 3 alisema Msama.
No comments:
Post a Comment