Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba
Moshingi, (kulia), akizungumza wakati wa kutiliana saini makubaliano ya
ushirikiano kati ya benki na baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi
jijini Dar es Salaam.
Na Mwandihi Wetu
BARAZA la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NDC), na Benki ya Posta Tanzania, (TPB),
wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha wanachama wa VCOBA ili
Akizungumza wakati wa
hafla ya kutiliana saini makubaliano nhayo kwenye ukumbi wa wizraa ya fedha
jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Beng’ Issa,
alisema, Katika juhudi za kuwawezesha watanzania kiuchumi kupitia upatikanaji
wa mitaji na kuendeleza ujasirimali nchini, Serikali kupitia Sheria ya Taifa ya
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, ibara ya IV, sehemu ya 16 iliagiza
uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Mwanachi yaani ‘’Mwananchi
Empowerment Fund,”.
“Katika kukabiliana na
changamoto ya ukosefu wa mitaji yenye gharama nafuu kwa wajasiriamali nchini,
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limesaini hati za makubaliano
na Benki ya Posta Tanzania katika kusimamia udhamini wa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi mbali mbali
ya wajasiriamali nchini yanayokidhi masharti husika.” Alisema Beng Issa.
Mfuko huu utakao simamiwa
na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni pamoja na kutoa fursa kwa
wananchi katika makundi au mtu mmoja mmoja kupata mitaji ya kuwekeza kwenye
miradi ya kiuchumi kupitia mikopo ya moja kwa moja au udhamini (direct lending
or guarantee system).
Ili kutimiza azama hiyo
baraza limeamua kushirikiana na benki ya ;posta Tanzania ambayo ina mtandao
mpana, kutekeleza azma hiyo ambapo wananchama wa VICOBA, watapata mikopo na
mafunzo kutoka benki ya posata.
Kwa aupande wake,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, alisema, benki
yake ni benki ya wananchi na hivyo unayo
furaha kubwa kushirikiana na NE, ili kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kupata
mikopo itakayowazsaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
“Benki ya Posta inayo
furaha kubwa kushirikiana na Baraza hili ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi
kupata huduma za kifedha kwa gharama nafuu kupitia mpango huu.” Alifafanua Moshingi.
Alisema, Benki ya Posta
inaamini kuwa hii ni fursa muhimu kwa vikundi hivi visivyo rasmi kufungua akaunti na kuweka fedha zao mahala
salama. Hili litawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi, na hatimaye
wataweza kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Hadi sasa
Benki imefungua zaidi ya akaunti 340 za vikundi. Vikundi hivi vitafaidika pia
na huduma ya TPB POPOTE, itakayo wawezesha kupata huduma za kifedha popote pale
walipo.
No comments:
Post a Comment