NA KENNETH NGELESI, TUNDUMA
DIWANI aliyemaliza muda wake katika Kata ya Tunduma kupitia Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frank Mwakajoka (pichani) amewaaga
wananchi wa kata hiyo huku akiwaasa wananchi kuwaenzi watumishi
serikali katika idara mbalimbali ikiwemo Sekta ya elimu ili kusaidia kumaliza
matatizo yaliyopo.
Wito huo imetolewa hivi karibuni na Diwani huyo katika mkutano wa
hadhara ambao ulikuwa kwa ajili ya kuwaaga wananchi wa kata hiyo uliofanyika Uwanja
wa shule ya Msingi Mwaka mjini Tunduma,ikiwa ni siku tano tangu baraza la
Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Mbeya kuvunjwa.
Mwakajoka alisema kuwa ni vema wananchi wakatoa ushirikiano wa
hali na mali kwa watumishi hasa katika sekta ya elimu ili kuweka mazingira
mazuri ya watoto kupata elimu kwa lengo la kata hiyo kuwa na maendeleo ya
kudumu katika kipindi hiki ambapo hakutakuwa na uwakilishi.
Akizungumza na mamia ya wananchi walifurika uwanjani hapo
Mwakajoka alisema Tunduma bado kuna unakabiliwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa nyumba za walimu, hali ambayo inawafanya watumishi hao
kutofanya kazi zao kwa utulivu hivyo ni vema wananchi wawe na ushirikiano mzuri
na watumishi hao ambao wanajukumu zito la kutoa elimu bora kwa watoto wao hivyo
ni kwao kusaixdia na Serikali kutatua changamotop hizo ikiwemo ya n yumba za
walimu.
“Ndugu zangu hawa walimu siyo kwamba kule waliko toka hawahitajiki
la hasha,bali wapo hapa kwa mjibu wa sheria lakini pia ndugu zangu wanatunduma
ni wajibu wetu kutoa ushirikiano kwao siyo kwa walimu tu bakli pia hata kwa
watumishi wa sekta nyingine ambao wapo hapa kwa jili kututumikia sisi lakini na
taifa kwa ujumla’alisema Mwakajoka.
‘Na ili tuweze na maendeleo endelevu ni lazima tuwaenzi walimu’ wanaowafundisha
watoto wetu, kwani tumefanya kazi kubwa ya kujenga vyumba vya madarasa na
kununua madawati, lakini bado walimu wetu wanachangamoto kubwa ya kupata nyumba
za kuishi, nawasihi tuwaenzi na kutoa ushirikano kwa walimu hawa kwa kutatua
changamoto zao,” aliongeza Mwakajoka.
Aidha katika hatua nyingine akizungumzia maendeleo ya
mji wa Tunduma, Mwakajoka alisema kuwa wakati akiingia madarakani
alikuta ukusanyajiwa mapato ukiwa wa chini huku ikitengwa bajeti
ndogo ya maendeleo ya kiasi cha shilingi milioni 800.
Alisema amekuwa akijitahidi kuibua vyanzo vipya vya mapato na
kudhibiti vilivyopo hali ambayo imeongeza mapato na bajeti ya mji huo hadi
kufikia zaidi ya shilingi bilioni 1.8 kwa mwaka.
Mwakajoka alisema kuwa kutokana na jitihada hizo, zilipatikana
fedha ambazo ziwezesha kujengwa kwa barabara nzuri kwa kiwango cha lami,
changalawe, na kuanzisha barabara mpya ambazo hazikuwepo kabla ya yeye kuingia
madarakani.
Aidha alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa
kujenga madaraja katika maeneo mbalimbali, barabara nyingi, vyumba vya
madarasa, visima vya maji, maabara kwenye shule za sekondari, vituo vya afya na
zahanati.
Diwani Mwakajoka alisema kuwa pia amefanikiwa kupandishwa hadhi
kwa mji wa Tunduma ambao ameingia madarakani ukiwa ni kata, lakini
sasa anapostaafu mji huo umekuwa Halmashauri kamili inayojitegemea.
Alisema kuwa kwenye uchaguzi Mkuu ujao kata ya Tunduma pekee
itagawanywa katika kata 12 na nyingine tatu za pembezoni mwa mji zitaongezwa na
kuifanya Halmashauri ya Mji wa Tunduma kuwa na kata 15.
Aliwataka wananchi wa Tunduma kuichagua Chadema kwenye
kata zote ili kukiwezesha chama hicho kuunda halmashauri ambayo itaendeleza
mambo mema aliyoyaanzisha na kuyaacha kabla hayakamilika.
Alisema mpaka anastaafu
ameacha bajeti ya ya Halmashauri hiyo ya shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika
kuleta maendeleo kupitia kwenye miradi mbalimbali.
Kwa upande Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
ya Chadema, Harod Jivava alisema kuwa baada ya kazi nzuri ambayo imefanywa na
diwani huyo, sasa nia ya chama hicho ni kupata madiwani wengi zaidi
wakatakaounda Hamlashauri ya mji wa Tunduma kwa lengo la kuwaletea
wananchi maendeleo zaidi.
No comments:
Post a Comment