HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2015

LUKUVI APAMBANA NA MIGOGORO YA ARDHI DAR ES SALAAM

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa Dar es salaam waliokuja kuwasilisha malalamiko yao kuhusu migogoro ya ardhi, kulia ni naibu wake Mhe. Angela kairuki na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Methew Nhonge, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt.  Selasie Mayunga na Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka.
Waziri wa Ardhi akipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi akipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Wananchi wa manispaa ya kinondoni wakiwa katika mkutano huo.

Na Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akutana na wananchi wa Dar es salaam na kupokea malalamiko ya migogoro inayohusu ardhi katika mkoa wa Dar es salaam tarehe 22 na 23, septemba, 2015 kuanzia saa 4.00 asubuhi makao makuu ya Wizara hiyo.

Katika siku ya jana tarehe 22 septemba 2015 Mhe. Waziri amepokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya kinondoni na leo tarehe 23 septemba 2015 atapokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Temeke na Ilala.

No comments:

Post a Comment

Pages