Sam Mapenzi pamoja (kulia) akiimba pamoja na Ashura Kitenge wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika siku ya Jumapili kwenye kiota cha Escape One Mikocheni na leo sio ya kukosa njoo tukeshe pamoja tukifurahi na mziki mzuri kutoka katika bendi hiyo.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba huku mashabiki wa bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako uje kuona vitu vipya kutka kwenye bendi hiyo.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha akiendelea kutuoa burudani kwa mashabiki wao waliofika kwenye kiwanja cha Escape One kujionea burudani ya nguvu kutoka katika bendi hiyo.
Msanii wa Bendi ya Skylight, Sony Masamba akiwafundisha mashabiki wao style mpya ya kucheza nyimbo za Bendi ya Skylight.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Msanii wa Bendi ya Skylight Ashura Kitenge akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo(hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kuburudika na band hii.
Ilifika time ya Nigeria Flavour Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kushoto) pamoja na Sony Masamba.
Ilikuwa noma sana siku ya Jumapili iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo Jumatano kwenye mkesha wa EID uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
No comments:
Post a Comment