Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto) akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza Tanzania imetangaza udhamini wake wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 kilomita 10 kwa walemavu.
Akitangaza udhamini huo wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu.
“Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tuanze kudhamini mwaka 2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mashindano haya,” alisema Kakwezi.
“Kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo wanashiriki walemavu pekee,” alisema.
Alisema udhamini wa GAPCO pia utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na pia zawadi za pesa kwa washindi wa mbio hizo za kilomita 10 ambazo zinafanyika pamoja na mbio nyingine za Kilimanjaro Marathon.
Kakwezi aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”
No comments:
Post a Comment