HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 28, 2026

MWENYEKITI WAZAZI TAIFA AMPA KONGOLE DED MANISPAA YA KIBAHA MJI KUTENGA ML.280 UJENZI WA ZAHANATI

Na Victor Masangu, Kibaha


Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Wazazi CCM Taifa Ndg Fadhili Maganya amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Kibaha Dkt Rogers Shemwelekwa kwa kutekeleza ilani ya chama  kwa vitendo  kwa  kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo  kupitia mapato yake ya ndani.


Pongezi hizo amezitoa  wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  yenye lengo la  kuweza  kuangalia uhai wa  chama cha mapinduzi (CCM) ikiwa sambamba  na  kuimarisha jumuiya zake  zote za vijana, wazazi, na wanawake na kufuatilia utekelezji wa Ilani  ya chama.



Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo ambaye pia ameweza kupata fursa ya kutembelea mradi wa Zahanati ya Kilimahewa ambapo ameridhishwa kuona ujenzi wa majengo yaliyopo yamejengwa katika kiwango kinachotakiwa na kwamba fedha  zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 285 zimetokana na mapato ya ndani.


"Nampongeza kwa dhati Mkurrugenzi mtendaji wa Manispaa ya Kibaha mji Dkt. Rogers Shemwelekwa kwa kuweza kuchapa kazi kwa bidii katika  suala zima la utekelezaji wa ilani kwa vitendo kwani ameweza kutekeleza baadhi ya miradi kwa kutumia fedha za mapato ya ndani nampa hongera sana,"amebainisha Mwenyekiti wa Wazazi Taifa

 

Pia Mwenyekiti  huyo akiwa katika mkuitano wake wa ndani na viongozi wa CCM pamoja na jumuiya za ke ambao umeefanyika katika shule ya Uongozi  ya mwalimu Julias Nyerere amempongeza  Mkurugenzi huyo kwa uwajibikaji na  kusimamia vema   utoaji wa mikopo ya asilimia 10  ambayo inatolewa na Halmashauri.


"Nimeridhishwa na huduma mnayotoa, nimeona mna idadi nzuri ya watumishi pia vifaa tiba sambamba na maji jambo ambalo ni muhimu sana katika zahanati, naipongeza Manispaa na nampongeza Mkurugenzi kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kujenga Zahanati hii kwa kutumia mapato ya ndani," amesema Maganya.


 Maganya akizungumzia  suala la zima la utoaji wa fursa za  mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa, Maganya amesema pamoja na kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata mikopo hiyo isiyokuwa na riba bado kuna jukumu la kushuka chini zaidi ili kuwafikia wananchi wengi.


 "Kitu kikubwa  mkurugenzi pamoja na kufanya kazi nzuri sana katika mambo mbbali mnbali lakini  kwa sasa hakuna  budi kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kupunguza malalamiko yanayotolewa na wananchi, nataka nione hii idadi uliyosema ya wajasiriamali 3000 vikundi 457 vinaongezeka na kuwa vingi zaidi"

Maganya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt Shemwelekwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushirikiana na Viongozi wa CCM Wilaya ili kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri baina ya Chama  pamoja na  Serikali.


Kwa upande wa Mkuu wa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt Shemwelekwa amesema katika kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inafika kwa wananchi yeye pamoja na tilmu yake walienda kwenye Kata 7 za Manispaa kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na vikundi vya wajasiriamali ili kuweza kupata mikopo hiyo isiyokuwa na riba.


"Mimi na timu yangu tulifika katika Kata 7 za Manispaa, tukatoa elimu ya mikopo na hadi kufikia mwaka 2026, tumevifikia vikundi zaidi ya 457 sawa na wajasiriamali 3,000 waliokidhi vigezo na tumewapatia mikopo hiyo na wanairudisha kwa wakati ili wananchi wengine waendee kuchukua,"amesema Dkt Shemwelekwa.


Ameongeza kuwa, wamekuwa na utaratibu mzuri wa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi katika matukio yote na hata kwenye utoaji wa mikopo hiyo wa vikundi wamekuwa bega kwa bega katika kuimarisha mahusiano ya Chama na Halmashauri kwa ujumla.


Kwa upande  wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe, Silvestry Koka amesema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kwa lengo la kuweza kuendelea kukusanya mapato kwa lengo la kupata fedha ambazo zitatumika katika miradi mbali mbali ya maendeleo.


"Mimi kama Mbunge wa Jimbo hili nitahakikisha naendelea kushirikiana kwa dhati na watendaji wengine pamoja na mkurugenzi na lengo kubwa ni ni kuendelea kuwaletea wananchi chachu kubwa ya kimaendeleo na mimi nampongeza sana Mkurugenzi wetu Dkt. Rogers Shemwelekwa kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya ukusanyaji wa mapato ya ndani," amebaainisha Mbunge Koka.


Naye Meya wa Manispaa ya Kibaha Mjini  Mhe. Dr Nicas Mawazo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazinkubwa anayoifanya na kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa ya Kibaha.


Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  kwa upande wa suala la utoaji wa fursa za  mikopo ya asilimia 10,  kwa makundi ya vijana, walemavu na wakinamama hadi kufika mwaka 2026 imefanikiwa kutoa kiasi   cha  jumla ya Shilingi bilioni 3.1 katika  vikundi   vipatavyo 457.

No comments:

Post a Comment

Pages