Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Balozi Olivier Nduhungirehe, leo, tarehe 26 Julai, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao walijadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na maendeleo kati ya Tanzania na Rwanda, pamoja na masuala yenye maslahi ya pamoja katika ngazi ya kikanda na kimataifa, ikiwemo uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Rusumo unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania, Rwanda na Burundi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Bujiku; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo, Bi. Julieth Muchunguzi; na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Balozi Olivier Nduhungirehe aliwasili nchini Julai 25, 2026 kwa ziara ya kikazi.



.jpeg)




No comments:
Post a Comment