Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani.
Wadau wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga (hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani, Jackson Kalikumtima (kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment