WATANZANIA
wametakiwa kuwapelewa watoto wao katika vyuo mbalimbali vya ufundi
stadi elimu inayo zalisha ajira nyingi kuliko vyuo vikuu hapa nchini ili
kuepukana na tatizo la ajira.
Inadaiwa kuwa watu
wanaojiajiri wengi wao wanatoka katika vyuo vya ufundi kuliko wanaomaliza vyuo vikuu kutokana na sababu hiyo wahitimu wengi kutoka vyuo vikuu wanategenea
kuajiliwa huku wa vyuo vya ufundi wakijikita kujitengenezea ajira na
kuachana na utegemezi kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo
imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Veta kamda ya nyanda za juu
inayo jumuisha mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe, Kabaka Ndenda, juzi
katika mahafari ya kwanza kwenye chuo pekee ya wilaya cha Veta Makete,
alisema kuwa vijana wengi wanao maliza katika vyuo vya ufundi
wanauhakika wa kujiajiri kuliko wanao enda vyuo vikuu.
Alisema
kuwa wananchi wamekuwa wakiona ni bora kumpeleka mtoto wake katika chuo
kikuu kuliko kumpeleka katika vyuo vya ufundi, alisema kuwa Tanzania
kutokana na ulivyo mfumo wa ajira watoto ni bora wakapelekwa katika vyuo
vya ufundi ili kutengeneza ajira.
"Tanzania tulikataa
mfumo wa mwalimu Nyerere wa ujamaa tukataka ukabaila wakati hatuwezi
kwenda nao ndio maana tunapata shida kupata ajira, Tanzania bado
hatujafika hatua ya kusoma vyuo vikuu na kupata ajira moja kwa moja,"
alisems Ndenda.
Alisema kuwa licha ya vijana hao wanao
fuzu mafunzo kuweza kujiajiri wanatakiwa kuhakikisha kuwa wakitoka hapo
wanaenda kuunda vikundi ili waweze kukopesheka.
Hata
hivyo wanafunzi hao waliiomba serikali kuhakikisha kuwa inawapa sapoti
pale watakapo kuwa wameunda vikundi vyao na kuweza kujikwamua kimaisha
kwa kupata mikopo kutoka serikalini.
Mkuu wa chuo hicho
Ramadhani Sebo alisema kuwa wanafunzi hao wanaenda kuajirika licha ya
kuwa na changamoto za vifaa vya kufundishia katika baadhi ya fani zinazo
fundishwa katika vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na katika fani ya ufundi
magari.
Alisema kuwa wanafunzi katika chuo hicho
wamefanya mafunzo kwa vitendo na wameiva vyakutosha kwenda kuingia
katika kujiajiri katika ufundi na kuanza kujitegemea.
Alisema
kuwa chuo hicho kwa sasa ambacho ni chapekee cha wilaya Tanzania nzima
na kuwa kilianza na kozi mbili na sasa kina kozi 4 huku kikifundisha
masomo mtamboka.
Alisema kuwa kutokana na kuto kuwa na
mabweni chuo hicho wanafunzi wake wamepanga mitaani na kuwa baadhi ya
wanafunzi wameshindwa kumaliza chuo kutokana na changamoto za kutoka
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment