HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2015

WENGI WAZIMIA MSIBA WA MAWAZO, KUZIKWA KIJIJINI KWAKE NOVEMBA 30

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa  akihutubia waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Geita, marehemu Alphonce Mawazo kwenye Uwanja wa Mnada wa Ng'ombe mjini Katoro jana. Uwanja huo ulibatizwa jina la Mawazo. (Picha zote na Sitta Tuma) 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwafariji waombolezaji waliojitokeza katika eneo la Katoro mjini, mahali alipouawa marehemu Alphonce Mawazo.
 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili  wa marehemu Alphonce Mawazo wakati wa ibada ya kuaga mwili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza mjini Geita.

Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili  wa marehemu Alphonce Mawazo wakati wa ibada ya kuaga mwili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza mjini Geita.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wameanguka na kupoteza fahamu wakati wa kumuaga marehemu Alphonce Mawazo kwenye Uwanja wa Magereza mjini Geita.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono waombolezaji baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Alphonce Mawazo kwenye Uwanja wa Magereza mjini Geita.

No comments:

Post a Comment

Pages