Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, wakati akimtangaza Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu
kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25 kwenye
ukumbi Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Khamis Pembe. (Picha na Francis Dande)
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi katika Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25 kwenye ukumbi Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Khamis Pembe akitoa ufafanuazi kwa waandishi wa habari jinsi walivyojiandaa katika tamasha hilo hususani kuhusu ulinzi.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi katika Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25 kwenye ukumbi Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Khamis Pembe akitoa ufafanuazi kwa waandishi wa habari jinsi walivyojiandaa katika tamasha hilo hususani kuhusu ulinzi.
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amekubali kubeba hadhi na heshima ya Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.
Akithibitisha hilo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya inayoratibu tamasha hilo lililobeba maudhui mengi kwa pamoja, Alex Msama alisema wanashukuru kiongozi huyo kukubali kubeba heshima hiyo ya muziki wa injili.
“Tunamshukuru mama yetu mpendwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kukubali kwa moyo mweupe kutuunga mkono akiwa mgeni rasmi.
“Ni heshima kubwa kwa Tamasha hili na malengo yake Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,” alisema Msama.
Alisema, mbali ya Tamasha hilo kuwaleta wapendwa kufurahia pamoja kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, pia litatumika kumshukuru Mungu kuijalia nchi kupita salama
katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Msama alisema zaidi ya hayo, pia wateule wa Mungu siku hiyo watakuwa na maombi maalumu ya kumuombea Rais Dk. John Pombe Magufuli na serikali yake azidi kuwa mzima na mwenye afya njema, hekina, maarifa na busara katika kukidhi matarajio na malengo ya Watanzania.
Alisema mbali ya maombi maalumu ya dakika 10 ya kumuombea Rais Magufuli na serikali yake, kupitia tamasha hilo litakalopambwa na waimbaji nguli wa kitaifa na kimataifa, sehemu ya fedha zitaendelea kuyafariji makundi maalumu kama walemavu, yatima na wajane.
Msama alisema pia, idadi ya waimbaji ambao watatumbuiza katika Tamasha hilo ambalo limezidi kuwa gumzo, imeongezeka baada ya mwimbaji nguli wa Tanzania anayeishi Kenya, Faustine Munish naye kuthibitisha.
Waimbaji wengine wa kimataifa, ni Rebecca Malope wa Afrika Kusini, Ephraem Sekereti (Zambia), Sarah Kierie (Kenya) na wengine wengi wa hapa nchini wakiongozwa na Rose Muhando.
Alisema, Munish mmoja wa waimbaji mahiri nchini wa nyimbo za injili kushiriki tukio hilo, kunazidi kuongeza uzito kutokana na nyimbo zake kubeba ujumbe unaowagusa wengi kwa kipindi chote cha huduma yake.
No comments:
Post a Comment