Wafanyakazi wa Mgahawa wa Armani wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakiwa makini kupata maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa wa mgahawa huo,Bi. Liu Li (katikati),juu ya kutoa huduma bora kwa wateja.Mkurugenzi huyoamedai kuwa wamedai kuwa mafuriko hukoseha migahawa mapato .Mpigapicha wetu aliwanasa kwenye mgahawa huo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Halmashuri ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imelalamikiwa kwa kushindwa kusafisha mifereji inayosabisha mafuriko wakati wa mvua, jambo linalodaiwa kukosesha mapato katika migahawa mingi jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa mgahawa wa Armani Bi Liu Li amedai kuwa kumekuwa na matatizo ya mifereji kufurika na kusababisha wateja kushindwa kufika katika eneo lake la Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako anakoendesha shughuli zake za kuhudumia vyakula wateja wake.
Amewashauri wahusika kuona umuhimu wa kuwa na mazoea ya kusafisha mifereji mara kwa mara kwa ajili ya kuepusha mafuriko yanaokumba eneo hilo la Mikocheni.
Bi
Liu Li ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa mgahawa huo amebainisha kuwa sekta ya migahawa ni moja ya sekta nyeti na inatoa ajira kubwa kwa vijana ambao wengi wamekosa kazi katika maofisi ya serikali.
Ameddai kuwa katika mgahawa wake wa Armani ukiwa na maana ya kudumisha amani, umeajiri zaidi ya vijana 40 na mpango wake wa baadaye ni kuajiri vijana wengi zaidi endapo kutakuwa na uboreshaji wa miundo mbinu katika eneo hilo la Mikocheni.
Mkurugenzi huyo amedai kuwa wateja wengi hushindwa kufika katika eneo la mgahawa wake kutokana na mafuriko ya mara kwa mara yanayosabishwa na mifereji michafu.
Bi Liu Li ametaja changamoto ningine kuwa ni uchakavu wa barabara zinazoelekea katika mgahawa wake na amewashauri wahusika kufanya matengenezo ya mara kwa mara kwa barabara za jijijni Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo Mtendaji pia ametupia lawama uongozi wa Tanesco kwa kushindwa kudhibiti kukatika kwa umeme mara kwa mara.
“Vyakula vingi vinaharibika na kutupwa, hii hasara kubwa kwa wamiliki wa migahawa hapa Tanzania” amelalamika Mkurugenzi huyo
“Sisi tunapenda amani hata jina la mgahawa wetu ni Armani “amesema Liu Li na kuongeza kuwa “sasa biashara yetu haina amani kabisa hapo”.
Amependekeza uongozi mpya na wizara ya Nishati na Madiani kuchukua hatua na kuweka mikakati ya kutosha ya kuondoa tatizo sugu la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Wakazi wa Mikocheni na Msasani waliohojiwa wamedai kuwa uongozi wa Halmashauri ya Kinondoni hauonyeshnia dhabiti ya kuondoa tatizo la mafurika eneo la Mikocheni na Msasani jijini Dar es Salaam
Wameomba mamlaka ya seikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuwawajibisha viongozi wa halmashauri ya Kinondoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgahawa huo waliohojiwa wametaka halmashauri ya Kinondoni kuchapa kazi na kuondoa tatizo sugu la mafuriko katika eneo hilo.
Kiongozi wa wafanyakazi hao Castory Alex wateja wakiwa wengi vijana wengi hupata ajira katika migahawa mingi jijini lakini mafuriko husababisha vijana wengi kukosa ajira.
Alex ameshauri kuwa halmashauri ya Konondoni inaweza kutenga siku ya Jumamosi kuhamasisha wakazi na wafanyakazi wa eneo hilo kujitolea kusafisha mifereji na kuondoa tatizo la mafuriko.
No comments:
Post a Comment