WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu
(kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya
Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada
ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la
Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa MSD wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. UmyMwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni.
Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia katika mikoa ya Arusha naMbeya, kwani hicho ni moja ya kipaumbele katika uongozi waserikali ya awamu yaTano.
Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasa kufika hadi asilimia 95.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema maduka mawili ya Arusha naMbeya yamemekamilika, na yanatarajia kufunguliwa hivi karibuni, na kwamba kwa mikoa mingine wameshafanya mawasiliano na kwamba tayari MSD imefanya mazungumzo na viongozi wa mikoa Ruvuma, Rukwa, Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa kufungua maduka yao ya dawa ambapo MSD itawauzia dawa.
“Tutakachofanya, sisi (MSD) utawapa utaalamu na kuwawezesha utaalamu wa uendeshaji maduka hayo” alieleza Bwanakunu.
No comments:
Post a Comment