Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewataka wanavyuo nchini kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Aliyasema hayo mjini Dodoma juzi wakati akizindua mpango wa Akiba na Afya ‘AAPLUS’ kwa wanavyuo, ambapo alisema kufanya hivyo itakuwa ni vyema kujiwekea mazingiria ya kujikusanyia mtaji kupitia NSSF ili mtu amalizapo chuo aweze kuwa na cha kuanzia katika kujiajiri.
Alisema hatua hiyo inatokana na ajira rasmi kuwa chache na wanaomaliza vyuo ni wengi hivyo kupitia mpango wanavyuo wengi watanufaika.
Pia alisema Shirika la NSSF limeahidi kuwafikia na kuwaunganisha wanavyuo wote katika mpango huo na wale ambao hawana ajira rasmi hivyo ni wajibu wao wanavyuo kuchangamkia fursa hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Mariam Ahmed alisema mpango huo ni muendelezo wa dhamira ya Shirika kupanua wigo wake kuwafikia watu wengi zaidi.
‘Ikiwahusisha waliojiajiri wenywewe na hata wanafunzi wa vyuo kwa mpango wa kujiunga kwa hiari na kuchangia kiwango kisichopungua Sh. 20,000 kwa kila mwezi ili kupata matibabu ya bure na mafao mengine yatolewayo na NSSF’.
Pia Meneja wa NSSF, Mkoa wa Dododma,Rehema Chuma amesema kwa wanafunzi ni mpango ambao utawawezesha kupata matibabu ya bure huku fedha yao ikiwa haijapunguzwa chochote licha ya mtu kuwa ametibiwa’.
Aidha mshauri wa wanafunzi wa UDOM, Dick Manongi amesema kuwa wanafunzi watakaojiunga na mpango huo wana faida kubwa kwa kuwa watatibiwa katika hospitali iliyopo hapo chuoni na hawatalipa tena hela ambao awali kabla ya kujiunga na NSSF ilibidi kujigharamia matibabu.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto) akimkabidhi mfano wa kadi ya uanchama wa NSSF, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rajabu Mahumba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa AKIBA na AFYA 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo hafla hiyo ilifanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akipeana mkono na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo, uliofanyika UDOM. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Mariam Ahmed.
Meza Kuu.
Wanafunzi.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo.
Baadhi ya waafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dick Manongi akizungumza katika uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango wa NSSF wa Akiba na Afya kwa Wanafunzi wa Vyuo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo.
Mwanafunzi wa UDOM, Mishi Jumanne akiuliza swali kuhusu uanachama wa NSSF.
Wanafunzi wakipimwa afya katika viwanja vya chuo cha UDOM.Dk. Leilah Manga wa Kituo cha Afya Chuo Kikuu cha Dodoma akipima mapigo ya moyo ya mwanafunzi wa UDOM, Hoza Ernest
Wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na NSSF.
Ofisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Issa Salim (kulia) akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliojiunga na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo, Abubakar Soud (katikati) akiwaelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa uzinduzi wa mpango wa Akiba na Afya 'AAPLUS' kwa wanafunzi wa vyuo uliofanyika katika chuo hicho, mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiagana na Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF, Abdul Mzee.
No comments:
Post a Comment