Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI wa nyimbo za Injili Tanzania, Sifael
Mwabuka na Goodluck Gozbert wamethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka 2016
linalotarajia kufanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi
ya tamasha hilo, Alex Msama
waimbaji hao ni muendelezo wa kufanikisha tukio hilo linalotarajiwa
kufanyika mikoa ya Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).
Msama,
alisema wanaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kukemea mauaji ya
walemavu wa ngozi ‘albino’ kupitia waimbaji wa muziki wa Injili watakaopanda
jukwaani siku hiyo.
Msama
alitoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwa sababu sehemu ya
mapato ya tamasha hilo
yanalengwa kusaidia kununulia baiskeli zaidi ya 100 za walemavu ambazo zitagawiwa kwa wahusika.
Aidha,
Msama alitaja viingilio katika mchezo huo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na
shilingi 2000 kwa watoto.
Msama
alisema hivi sasa waimbaji mbalimbali waliothibitisha kushiriki tamasha hilo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa
kabla ya tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment