HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 27, 2016

WATUMIAJI MITANDAO YA KIJAMII KUHOJIWA

Na Talib Ussi, Zanzibar

Jeshi la Polisi Zanzibar  linakusudia kuwahoji watumiaaji wa mitandao ya kijamii 34 kutokana na kuhamasisha vurugu sambamba na kuandika lugha za matusi zinazowalenga viongozi wakuu hapa visiwani.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI) Salum Msangi (pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.

Alisema kuwa mara baada ya kufutwa kwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, kumejitokeza baadhi ya watu na vikundi mbali mbali vinavyotumia mitandao ya kijamii kwa kuandika maneno ya matusi au kutoa clip za kuongea zenye lugha ya matusi kwa kuwatukana watu mbali mbali hasa viongozi wa kitaifa.


 Alisema  kuwa uchunguzi wa kitaalamu na kisayansi unaendelea na utakapokamilika jalada la ksi hiyo litapelekwa  kwa Mkurugenzi wa Mashataka (DPP) ikiwa ni utaratibu wa kupeleka kesi mahkamani.

Alisema     kwamba jeshi hilo limepata  orodha ya watumiaji  hao na hadi  sasa Jeshi la Polisi linamhoji mtu mmoja kwa ajili  uchunguzi ambae anatuhumiwa kutoa moja ya clip  zenye lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Msangi alitoa tahadhari kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kwani kutumia lugha za matusi ni kosa lililoainishwa kisheria kwenye sheria ya kanuni ya adhabu na yoyote atakaefanya kitendo hicho atakamatwa na kufikshwa mbele ya vyombo vya sheria, bila ya kujali limetolewa mahala gani au wakati gani.


“wasidhani kwamba demokrasia ni kuwatukana vuiongozi hilo wasijidanganye  lazima sheria ichukue nafasi yake” alisema Msangi.


Aliwatahadharisha  watumiaji wa mitandao kwamba serikali iko macho na matendo yao na kuwataka kuacha mara moja kutumia mitandao kwa kukashifu viongozi au watu wengine.


“kabala mtu hajaandike apime ni kitu gani ambacho anataka kuandika kwani akienda kinyume tutamshuhulikia” alieleza Msangi.


Hivi  Karibuni aliyekuwa mmoja wa Timu ya ushindi ya Chama cha wananchi CUF alikamatwa wiki iliyopita kwa madai ya kutoa klip ambayo anamtukana rais wa Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

Pages