HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 27, 2016

DIWANI WA CCM AZIKWA

NA TUMAINI MAFIE, ARUMERU

MAZISHI ya aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngarenanyuki kupitia chama cha mapinduzi  CCM  Naftal Mbise yalifanyika  jana  nyumbani kwake Wilayani Arumeru mashariki iliyopo jiji la Arusha.

Aidha marehemu Mbise ambaye kifo chake kilitokana na kuanguka kwenye mti  aliokuwa akipunguza matawi machi 21 ameacha pengo katika  Kata yake  kwani alikuwa Diwani pekee wa CCM kwa jimbo  hilo.

Akisoma historia  ya marehemu ndugu wa karibu wa marehemu alisema diwani huyo alipanda kwenye mti  ili kupunguza matawi katika mti  uliokuwa  karibu na nyumba  yake  kwa kutumia ngazi ambapo baada ya kukata  tawi la kwanza alipoanza kukata  la pili ndipo  alipodondoka kutoka juu hadi chini nakupatwa na majeraha sehemu za ndani.

Alisema baada ya tukio hilo marehemu alikimbizwa katika kituo cha afya cha Ngarenanyuki na wauguzi kubaini kuwa yake  ni mbaya ndipo  alipokimbizwa hospitali ya wilaya ya Tengeru alipouguzwa mda mchache kabla ya mauti kumkuta.

Alisema enzi ya uhai wake Mbise aliwahi kuwa mwenyekiti wa kitongoji tangu  2004 hadi alipochaguliwa kuwa diwani Oktoba 25 mwaka jana  na kuongeza kuwa almbali na cheo hicho alikuwa  mlezi wa  timu ya mpira wa miguu ya Ngarenanyuki  hadi kifo chako.

Akitoa salamu  za rambirambi katika msiba huo Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassary alisema diwani huyo alikuwa mchapakazi bila kujali itikadi za chama aliwatumikia wananchi kwa moyo.

"Nilipata wakati mgumu niliposikia habari za kifo cha Diwani huyu ambaye alikuwa peke yake  katika chama cha CCM nilijiuliza nitasema nini  mbele ya wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki sijawahi kuishiwa na maneno lakini nakosa lugha ya kusema tumepoteza kiungo muhimu katika utendaji katika serikali yetu" alisema Nassary.


Alisema anayepaswa kuhukumu ni Mungu pekee na siyo mwanadamu kwani wanadamu wameumbiwa njia nyingi za kuondoka duniani.

Alisema halmashauri hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kuendelea kuleta maendeleo ya wananchi wa Kata hiyo ikiwa  ni pamoja na kuisaidia familia ya marehemu ili wasione napungufu ya kuondokewa na Mpendwa wao.

Tanzania daima ilishuhudia msiba huo  kuleta  gumzo kwa viongozi wa halmashauri ya Meru kutokana na ratiba mbili kukinzana katika hospitali ya Mkoa ya Mount meru baada ya taarifa mbili tofauti za utaratibu wa msafara wa kumpekeka marehemu huyo.

Awali ratiba iliyokuwa imepangwa na uongozi wa halmashauri hiyo ulionyesha msafara utaanzia mount meru na kuelekea katika makao makuu ya halmashauri ili wasioweza kuhudhuria katika mazishi waage mwili huo.

CCM nao walikuwa na ratiba yao ya msafara kutoka moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini  hapo kuelekea nyumbani kwa marehemu.

Jambo hilo lilileta mvutano kati ya viongozi wa halmashauri na  CCM ambapo baadaye mwenyekiti wa halmashauri hiyo  Willy Njau alimtaka Ofisa  tarafa ya king'ori Laanyuni Ole -Supuu kuwa kitu kimoja katika msiba huo na kusiwepo na mwingiliano kwa kuwa aliyefariki ni mtumishi wa serikali na siyo tu kuzikwa kiitikadi bali  taratibu za kiutumishi wa serikali zichukue nafasi katika msiba huo.

Hata hivyo tofauti hizo zilimalizika na hatimaye utaratibu wa msiba ulianza ambapo msafara ulienda kama ulivyokuwa umepangwa na halmashauri ambapo mwili uliagwa makao makuu ya halmashauri hiyo na baadaye kuelekea nyumbani kwa marehemu Ngarenanyuki.

Msiba huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwamo Mbunge wa jimbo  hilo Joshua Nassary,  wakuu wa wilaya hiyo na madiwani wa Kata zote za jimbo  hilo.
Marehemu ameacha mjane na watoto wadogo wawili wakiume. Chanzo Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

Pages