Kulia Mganga Mkuu
mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya
uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi
Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake walipokagua mazingira ya
hosptali hiyo leo. (Picha na Habari na Evelyn Mkokoi)
Katikati Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Bw. Charles Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa Iringa Bw.
Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja wakifanya usafi katika
soko la mji wa Iringa.
Kushoto Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais
Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi
sokoni Mkoani Iringa Leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mh. Luhaga Mpina Akipanda mti kabla ya
kuupanda , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.
Na EVELYN MKOKOI, IRINGA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa
Kulitaftia ufumbuzi suala la uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.
Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo alipotembelea Hosptali ya
Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika ziara
yake ya kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa maziringa
katika viwanda vya mkoa wa Iringa.
Imeelezwa kuwa uteketezaji wa tanga hatarishi katika hosptali
hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa
kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote
uliosababishwa na taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.
Kwa Upande wake mganga mkuu mfawidhi wa hospital hiyo dkt
Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina kuwa taka zizalishwazo katika
hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la mkoani hapo na hata
hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama
vile za sindano, gloves, nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.
Akitolea ufafanunuzi sualala za uteketezaji wa taka hatarishi
hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza
limewahi kushauri uongozi wa hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa
na kiwanda cha mbao cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda
hicho kina vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital
hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia
kuziharibu.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko
la Mjini Iringa na kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti,
ambapo Mh. Mpina,alipanda mti katika
kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa
taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake na kuwaasa
watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem
cha Kitwivu.
“Taifa lazima lipande miti ili kuhepukana na changamoto za
mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina
aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja
na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini
na tano kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment