Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi
Lugola, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. Kushoto ni mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana Shonza.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, akiongoza
kikao wakati Kamati hiyo ilipokutana na
Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Viongozi na Watendaji
Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es
Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati
meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu na kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu (wa tatu kulia), wakikagua mojawapo ya samani
za ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba
Yahya, ambazo zimetengenezwa na Jeshi la Magereza, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, akizungumza
wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
ilipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Alphonce Malibiche, akielekeza jinsi ya
kutambua taarifa sahihi za mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kwa wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati
Kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya
Nchi)
No comments:
Post a Comment