HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 05, 2016

UDASA WAMLILIA DK. RICHARD MGAYA ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI

 Dk. Richard Mgaya (wa pili kulia),  enzi za uhai wake.
Dk. Richard Mgaya (kulia), enzi za uhai wake wakati akiwa masomoni nchini Marekani.

Ndugu Wanaudasa,

Ninasikitika kuwataarifu habari za msiba wa Dk. Richard Mgaya wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta kilichotokea usiku wa kuamkia jana. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara (Dk. Honest Kimaro) kifo cha Dk. Mgaya kimesababishwa na ajali ya gari.

Siku ya jana kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii za gari lilipopata ajali eneo la Mbezi Afrikana baada ya kugongana na lori na kuwaka moto. 

Mashuhuda walishuhudia gari likiwaka moto na hivyo dereva aliungua moto na kuteketea na hakuweza kutambulika. Hivyo watu wakasambaza ujumbe kwa kutaja plate number za gari lililoungua ili kutafuta utambulisho wa dereva.

Kwa masikitiko makubwa, imejulikana kwamba dereva wa gari hilo alikua ni Dr. Richard Mgaya. Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta na jamii ya CoICT kwa ujumla imeshtushwa sana na msiba huu.

Dk. Mgaya alijiunga na idara yetu miaka kama minne hivi iliyopita akitokoea masomoni Marekani na alikua ni mtaalamu kijana wa Artificial Intelligence ambayo ni moja ya specialities za computer science zenye wataalamu wachache sana wa kiwango cha PhD hapa nchini mwetu (kama wapo zaidi ya yeye). 

Taarifa za kwamba aliyeungua kwenye gari hili alikua ni Dr. Mgaya zimeifikia familia yake leo mchana.

Pamoja na ujumbe huu, nimeambatanisha baadhi ya picha zilizopigwa eneo la tukio. Ni msiba mgunu sana kuuelezea na kuukubali.

Mungu mwenyewe awe faraja kwa ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na familia nzima ya UDSM.

No comments:

Post a Comment

Pages