HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2016

MAKABIDHIANO YA OFISI

Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini  akikabidhiana Ofisi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma Shangani  Mji Mkongwe wa Zanzibar, baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu).
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishiwa Umma na Utawala Bora  wakati wa makabidhiano ya Ofisi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma Shangani  Mji Mkongwe wa Zanzibar, baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment

Pages