HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2016

RAGE AJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

 RAIS wa zamani wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage, (kushoto), akipokea kadi yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, kutoka kwa Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa PSPF, Bi.Costantina Martin, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
 Alhaj Rage akionyesha kadi hiyo

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

RAIS wa zamani wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismael Aden Rage, amejiunga na mpangowa uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Aprili 14, 2016.

Rage ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tabora mjini, kufuatia kujiunga huko, amefaidika kuingizwa kwenye fao la huduma ya afya litolewalo na Mfuko huo kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambao una ushirikiano wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa PSPF wanaotaka kufaidikana huduma hiyo.

“Nitoe wito kwa wanamichezo wakiwemo wa mpira wa miguu, kuchangamkia fursa hiyo kwani mambo sasa yamebadilia kujiunga na PSPF kupitia mpango huu wa hiari ambao unamruhusu mtu binafsi au vikundi kujiunga na uanachama, lakini pia kutokana na kupanda kwa huduma za afya, ukiwa mwanachama wa PSPF unaweza kupata huduma ya afya wewe na familia yako, hii ni faida kubwa.” Alisema Rage wakati akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa PSPF, Bi. Costantina Martn.

Rage alisema, yeye kama mwanamichezo atahamasisha wanamichezo hususan wacheza mpira kujiunga na mpango huu kwani maisha ya sasa yanahitaji kwenda kisasa, na jambo muhimu ni kuwa na afya bora, na afya bora utaipata kama unapata huduma bora, nimeambiwa kupitia mpango huu ninaweza kupata matibabu kwenye hospitali yoyote nchini na wakati wowote, Alisema.

Awali Rage alijaza fomu za kujiunga na uanachama ambapo alipokewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe. Ambaye alimshukuru Rage kwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSSF), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akipokea fomu za kujiunga na uanachama kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016
 Alhaj Rage, (kushoto), akiweka dole gumba kwenye fomu yake ya uanachama huku akisaidiwa na Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw.Abdul Njaidi
 Alhaj Rage akijaza fomu, kuliani Bi. Mwanjaa Sembe
 Alhaj Rage, akikabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe, huku Njaidi akishuhudia.
 Rage akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe (kushoto)
 Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, akiwa mwenye furaha baada ya kupokea mwanachama mpya, Alhaj Ismail Aden Rage
 Alhaj Rage akipokewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Njaidi alipowasili kujiunga na Mfuko huo.
Alhaj Rage, akibadilishana mawazo na Bi. Costantina Martin, na Njaidi baada ya kuwa mawanachama wa Mfuko huo.

No comments:

Post a Comment

Pages