NA NEEMA
MWAMPAMBA
MFUMUKO wa
bei wa Taifa kwa mwezi machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia
5.6 ya februari 2016.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu(NBS), Albina Chuwa, alisema hali hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji
bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi machi,2016 imepungua
ukilinganisha na mwaka ulioishia februari 2016.
Alisema
Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 kwa mwezi machi 2016 kutoka 96.69
mwezi machi 2015 huku mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi
kwa mwezi machi 2016 umepungua hadi 8.3 kutoka asilimia 9.5 ilivyokuwa mwezi
februari 2016.
Alisema
kupungua kwa mfumo wa bei wa mwezi machi kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei
za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha mwezi machi 2016 zikilinganishwa
na bei za mwezi machi 2015.
“pamoja na
kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioishia mwezi machi
2016, kuna baadhi ya bidhaa zilizoonesha kuongezeka katika kipindi hicho zikiwa
ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 21.7, mahindi 47.8 na vyakula kwenye
migahawa 16.2”alisema Chuwa.
Akizungumzia
thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi machi Chuwa alisema Sh.100 ya
Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 98 na sent 11 mwezi
machi mwaka huu kutoka mwezi Desemb mwaka jana ikilinganishwa na shilingi 98 na senti 58 ya februari mwaka huu.
Pia alisema
mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za
Afrika Mashariki ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi machi nchini Kenya umepungua
hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.84 mwezi februari 2016 na Uganda imefika
6.2 kutoka 7.0.
No comments:
Post a Comment