HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2016

RAIS MAGUFULI AMFUKUZA KAZI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anne Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa.

Rais Magufuli hakuamini kama kuna Mkoa ambao hauna watumishi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi  ambacho hadi kufikia usiku wa kuamkia leo kimebaini wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli alikuwa anaongea baada ya kupokea ripoti ya Takukuru toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu, Valentino Mlowola, amesema amesikitishwa sana na kauli ya mama Malecela ambaye bila shaka amepata ushauri mbaya kutoka kwa watendaji wake.

Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili bado zilikuwa zinaendelea kuhakikiwa.

Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5,507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri. 

Hivyo pia, Rais ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdul Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa Mama Anne Kilango Malecela ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa Same Mashariki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita. 

No comments:

Post a Comment

Pages