Na Mwandishi Wetu
RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia Tawi la
CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina
nembo ya adamu na hawa wala bendera.
Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya saa saa nne asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika
makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.
Mara baada ya Rais
Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo
yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo.
Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja
waliyokuwa awakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo ilibidi wazuiwe kuingia
huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwisha ingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo
na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje
Rais kuingia benki kwa sitaili ile kwani baadhi ya wananchi kudai kuwa
hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva wa Tex, alisema baadhi ya
wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa
walishtuka lakini mara walimuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari hali
iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye
benki ya CRDB tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo tujui
kama hiyo ilikuwa inawezekana.
Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende akachukue fedha
kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu, alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki
hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi nwakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani
kwenye foleni nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini
hatukujua kilichomleta,”alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka
alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Rais John Magufuli akiwa ndani ya gari lenye namba za
usajili T182 DFQ huku akiwapungia mkono watu waliokuwa nje ya Benki ya
CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoka katika
benki hiyo. (Picha na Francis Dande)
Muuza maji (kushoto) akishangaa gari alilopanda Rais Magufuli leo asubuhi wakati akitoka Benki ya CRDB tawi la Holland.
Gari alilokuwa amepanda Rais John Magufuli lenye namba za
usaji T 182 DGQ likitoka katika benki ya CRDB tawi la Holland lililopo katika
makutano ya barabara ya Samora na Ohio jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment