SERIKALI
kupitia Wizara ya Maliasili
na Utalii imeshauriwa kuweka msukumo mkubwa kwenye kutangaza vivutio vya utalii
vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini kuweza kutumia fursa hizo
kukusanya mapato.
Ushauri huo
ulitolewa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kibanga Tours&Travel, Emanuel Kibanga
(Pichani kushoto) wakati
akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema ipo mikoa yenye fursa nyingi
za kiutalii lakini inashindwa kuonekana kutokana na kutotangaza
ipasavyo.
Alisema kuwa
iwapo suala hilo
litasimamiwa na kuchukulia hatua zinazokusudiwa itasaidia kuwapa ufahamu nzuri
watalii kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mikoa ya kanda ya kaskazini
ikiwemo Tanga kwa wingi kutokana na kuwepo na historia ya kubwa ya
kale.
“Ukiangalia mikoa ya Kanda ya Kaskazini inavivutio vyingi sana vya
utalii ukianzia na mkoa wa Tanga lakini vinakosa fursa ya kuonekana na wageni
wanaokuja kutembea hapa nchini na hivyo kuikosesha serikali mapato “Alisema
Mkurugenzi huyo.
Aidha pia
alitumia nafasi hiyo
kuushauri mkoa wa Tanga kuandaa kongamano maalumu ambalo litaweze kutoa fursa
za kutangaza vivutio vya utalii kwa lengo la kuongeza ukusanya
mapato.
Hata hivyo
alisema wakati umefika
sasa watanzania wawekeze kwenye maeneo yaliyokuwa karibu na vivutio vya utalii
ili kuweza kuhamasisha wageni kwenda kuvitembelea ili
kuharisisha.
Stori kwa Hisani ya Tanga Raha Blog
No comments:
Post a Comment