WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda kama
mkakati wa kukuza uchumi ili nchi iweze kutoka kwene umaskini na kufikia uchumi
wa kati.
Waziri Mkuu
amesema hayo leo (Alhamisi, Aprili 14, 2016) alipofanya mazungumzo na Waziri wa
Biashara wa Oman, Dk. Ali Masoud Al Sunaidy ofisini kwake Magogoni jijini Dar
es Salaam.
Amesema
mbali na kuimarishwa kwa sekta ya viwanda, pia Serikali imelenga kuboresha
sekta za nishati, uchukuzi na kilimo ambazo zitawezesha Taifa kufikia malengo
yake ya kufikia uchumi wa kati.
“Sekta ya
viwanda ni eneo ambalo tunataka kuliimarisha kwa sababu litatuwezesha kuongeza
thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini jambo ambalo pia litakuza ajira kwa vijana. Hivyo nawakaribisha mje
kuwekeza nchini,” amesema.
Pia Waziri
Mkuu amemuhakikishia kuwa serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji
wa kutoka Oman kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Kwa upande
wake, Dk. Al Sunaidy amefurahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na
kwamba wapo tayari kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo viwanda vya
usindikaji, kilimo kinachotumia teknolojia ya kisasa, na mafuta, gesi, na
ujenzi wa bandari.
Akitoa
ufafanuzi, Waziri huyo alisema: “Oman ina bandari ya Salala ambayo ni moja kati
ya bandari bora duniani yenye uwezo wa kupakua makontena 45 kwa saa. Lakini pia
tunayo bandari ya Sohar maarufu kwa bidhaa za viwandani ambayo ina uwezo wa
kupakua makontena 32 kwa saa,” amesema.
Dk. Al
Sunaidy yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu akiwa ameambatana na
wafanyabiashara 80 wa Oman kwa mwaliko wa Kiserikali kwa ajili ya kukuza
ushirikiano wa kiuchumi.
Naye Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema anatambua kuwa Oman
imepiga hatua katika teknolojia ya gesi asili ya kimiminika (LNG) hivyo ana
imani Tanzania itapata ujuzi kutoka
kwao.
Amesema
wafanyabiashara hao wana fursa ya kuwekeza kweye ujenzi ujenzi wa viwanda vya
mbolea katika mikoa ya Lindi na Mtwara lakini pia wanaweza kuwekeza kwenye
bandari za Tanga, Bagamoyo, Kilwa, Lindi na Mtwara ambazo Serikali imepanga
kuboresha miundombinu yake.
No comments:
Post a Comment