Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Uchukuzi SC na Tamisemi kesho zitacheza
mchezo wao wa mwisho wa netiboli, ambao ni kama fainali kutokana na timu zote
kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye
uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, kila mmoja akiwa na pointi tisa.
Netiboli inachezwa kwa mtindo wa ligi, ambapo timu
hizo zinakamilisha ratiba na mmoja akimfunga mwenzake atakuwa bingwa au zikitoka
sare ya idadi yeyote ya magoli, basi Tamisemi atatawazwa bingwa kwa kuwa anaidadi
kubwa ya magoli ya kufunga, 94 na wenzao wana 87.
Timu ya CDA Dodoma wanafuatia wakiwa watatu baada ya
kushinda mchezo mmoja, huku Tanesco na chipukizi wa TPDC wakimaliza mashindano
bila kushinda mchwezo wowote. Lakini TPDC inayofundishwa na kocha mzoefu Rose
Mkisi inayoundwa na wachezaji wenye umri mdogo kati ya 20-30, ndio timu changa
baada na inaonyesha baada ya mwaka mmoja itakuwa tishio kwani itakuwa na uzoefu
tofauti na sasa ndio wameanza mwaka huu kushiriki mashindano haya ya Mei Mosi.
Katika mchezo wa soka timu ya Geita Gold Mine
itakwaana na Tamisemi kesho katika mchezo wa fainali.
GGM wametinga hatua hiyo baada ya kuwafunga Tanesco kwa mikwaju ya
penati 4-2 baada ya kumaliza mchezo wa nusu fainali bila kufungana.
Penati zote nne za GGM zilifungwa na Gwetu Guvette, Oswald
Binamungu, Ally Twist na Mohamed, wakati za Tanesco walizopata ni Said Kondo na
Stan Uhagile, na walizokosa ni Hemed Mtumwa na Betwel Kagimbo.Nao Tamisemi
waliwachapa Uchukuzi SC kwa magoli 2-0.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa jana jioni Uchukuzi SC
waliwafunga chipukizi wa TPDC kwa magoli 33-14. Uchukuzi walikuwa mbele kwa
magoli 15-8.
Nayo Tamisemi waliwapeleka jamaa zao CDA na kuwachapa magoli 18-13.
Washindi walikuwa mbele kwa magoli 9-8.
Katika kamba kwa wanaume Ukaguzi waliwavuta CWT kwa mivuto 2-0,
nayo TPDC wakiwavuta UDOM mivuto 2-0, na Uchukuzi SC walipata ushindi wa chee baada
ya Tanesco kuingia mitini; wakati kwa wanawake Tamisemi waliwavuta bila huruma
Tanesco mivuto 2-0.
Mbali na netiboli na soka itakayochezwa kesho, pia kutakuwa mechi
za kamba wanaume TPDC kucheza na CWT, huku UDOM kuumana na Tanesco; wakati
wanaume Uchukuzi SC watakutana na TPDC.
Nahodha
wa timu ya Uchukuzi SC, Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa mchezo wa
nusu fainali dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mei Mosi,
Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni mkuu wa benchi, Kenneth
Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0.
Mwamuzi
Robert Mkatakiu (aliyeshika kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo
Ally wa Tamisemi aliyelala chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo
alionyeshwa kadi hiyo pamoja na nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia).
Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na Tamisemi wakisubiri mpira wa kona
upigwe na Omary Said wa Uchukuzi (haonekani pichani). Tamisemi walishinda
kwa magoli 2-0.
Kipa wa
Tamisemi,, Leonard Mkinga (katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake
kabla Uchukuzi hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli
2-0.
Tatu
Kitula (mwenye mpira) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga bao katika mchezo wa
netiboli wa mashindano ya Mei Mosi dhidi ya TPDC. Uchukuzi walishinda kwa
magoli 33-14.
No comments:
Post a Comment