Mkurugenzi wa Bagamoyo Historical Marathon,
Dominic Mosha akizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani
Pwani jana, wakati wa uzinduzi wa mbio
hizo, kwa mwaka 2016, zitakazofanyika Julai 24. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Riadha Tanzania (RT), Ombeni
Zavalla (wa pili kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Ayoub
Magimba na Mratibu wa mbio hizo, Dorah Raymond.
Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), Ombeni Zavalla (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, wakati
wa uzinduzi wa mbio za Bagamoyo Historical Marathon 2016, zitakazofanyika Julai 24. Wa (pili kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Prof. Ayoub Magimba, Mkurugenzi wa Mbio
hizo, Dominic Mosha (wa pili
kushoto) na Mratibu wa mbio hizo, Dorah Raymond.
NA MWANDISHI
WETU, BAGAMOYO
MBIO
za Bagamoyo Historical Half Marathon 2016, zinatarajiwa kufanyika Julai 24
mjini hapa na kushirikisha wanariadha kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Mbio
hizo za kila mwaka, zimeandaliwa na Kampuni ya 4Bel kwa lengo la kukuza vipaji
vya wanariadha chipukizi kutoka maeneo tofauti.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, Mkurugenzi wa 4Bel,
Dominic Mosha, alisema wamezindua rasmi mashindano hayo ili kuutaarifu umma na
kuwakaribisha kushiriki.
"Tumezindua
rasmi mashindano, tunaendelea na maandalizi kwa kasi,” alisema Mosha.
Alisema
zoezi la usajili na fomu kutolewa kwa ajili ya washiriki litaanza Julai 4,
ambapo wanawaalika washiriki kutoka mikoa tofauti wajitokeze kwa wingi.
Alisema
lengo lao safari hii ni kufanikisha kwa kiasi kikubwa na kuongeza kuwa,
wameboresha tofauti na miaka mingine iliyopita.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla,
alisema wamekubaliana na waandaaji wa mashindano hayo kwa sababu wana vigezo
vyote vya kuandaa ikiwemo kibali kutoka shirikisho hilo .
Alisema
mbio hizo zimekuwa mfano kwa waandaaji wengine kutokana na kuwa imekuwa ikilipa
zawadi kwa wanariadha kulingana na zile walizotangaza.
"Cha
msingi zawadi katika mashindano haya lazima ziwepo, ili kuepusha migogoro na
malumbano ambayo huwa yanajitokeza mara kwa mara endapo waandaaji wanaposhindwa
kutoa zawadi walizoahidi kwa washiriki,” alisema Zavalla.
Alisema
kutokana na hilo ,
wanapaswa kuandaa askari ambao watasaidia katika suala zima la ulinzi wakati
mashindano hayo yakiendelea.
No comments:
Post a Comment