Baadhi ya wazazi.
Mwalimu wa taaluma wa Shule ya Msingi Kumbukumbu, Fundikira akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya msingi Kumbukumbu.
NA NEEMA MWAMPAMBA
JAMII imeaswa kuacha
kuwatumikisha watoto katika biashra pindi wanapotoka shule nyakati za jioni na
badala yake wawapatie muda wa kujifunza.
Wito huo ulitolewa jana jijini
Dar es Salaamna mbunifu wa mavazi na Katibu wa Taasisi ya Binti Foundation
Kulthum Sadiq wakati alipokutana na wazazi watoto wanaosaidiwa na taasisi hiyo
kwenye shule ya msingi Kumbukumbu.
Mwanamitindo huyo alisema
alikutana na watoto wanaowasaidia kujua mambao yanayowakwamisha kufanya vizuri
ambapo wengi walilamikia kutumikishwa na wazazi wanapotoka shule.
Alisema ili mtoto afanye vizuri
na kufikia kama walipo watu maarufu
ulimwenguni lazima apate elimu katika mazingira bora.
Pia Binti foundation inatarajia
kutoa mikopo kwa wazazi wa watoto wanaowasaidia ili kuweza kufanya biashara
mbalimbali zitakazowawezesha kupata fedha za kuwahudumia watoto hao wanapokuwa
katika masomo.
"Tumeyasikiliza matatizo na
tutayachukua kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia fedha za kufanya
biashara mbalimbali zitakazowapa kipato muache kuwatumikisha
watoto"alisema Sadiq.
No comments:
Post a Comment