Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs. Milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei kwa ajili ununuzi wa madawati kwa shule za msingi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay na wa pili kulia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ukwamani, Winfrida Daudi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akiangalia mfano wa hundi ya Shs. milioni 100 aliyokabidhiwa na uongozi wa Benki ya CRDB kwa ajili ya ununuzi wa madawati Mkoa wa Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Meza Kuu.
Murugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake.
Dk.Kimei.
Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Kenneth Kasigila (kulia) akiwa katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kanda ya Dar es Salaam, Simon Siro.
Wanafunzi wakiigiza namna wanavyokaa wakiwa darasani. kulia ni mwalimu wao.
Meya wa Ilala, Charles Kuyeko (wa pili kushoto) akiwa na Meya wa Temeke, Abdalah Chaurembo (wa pili kulia).
Wanafunzi wakitumbuiza.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto).
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakitoa mchango wao.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakichangia.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakichangia.
Fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB papo kwa hapo zikihesabiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoa hotuba yake.
Mwanafunzi wa Shule ya SekondariUkwamani Kawe, Winfrisa Daudi akitoa Shukrani zake kwa niaba ya wanafunzi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kanda ya Dar es Salaam, Simon Siro. Katikati ni Mkuu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
NA IRENE MARK
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa Tsh. Milioni 100 kwaajili ya ununuzi wa madawati kwa shule za msingi zilizopo katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda, Dk. Charles Kimei alisema benki yake inatambua matatizo mbalimbaili yanayoikumba sekta ya elimu na ndio maana wameamuwa kutoa msaada huo.
Alisema kupitia sera ya msaada kwa jamii benki yake imekuwa ikitoa misaada mbalimabli katika sekta ya elimu na kuelekeza nguvu zake katika kujenga madarasa, mabweni, maktaba pamoja na ununuzi wa vitabu.
“Sisi ni wadau wa kwanza wa kuchangia ujezi, upanuzi na uboreshaji wa vyuo vikuu nchini ambapo pamoja na mambo mengine benki pia imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo ya kazi kwa wanafuzni zaidi ya 5000 kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uzoefu wa kazi,” alisema Kimei.
Aidha alisema kwa mwaka huu benki hiyo itakuwa ikijikita zaidi katika kuisaidia sekta ya elimu ikiwa ni harakati za kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Naye Mkuu wa Mkoa, Makonda alisema anaishukuru benki hiyo kwa msaada huo kwani utakwenda kuwasaidia wanafunzi zaidi ya 4,500 waliokuwa wakikaa chini kutokana na ukosefu wa madawati. “Msaada huu unatupa faraja kubwa sana ya kuwa wapo watanzania na taasisi zinaguswa na maendeleo ya elimu nchini, naomba nikuhakikishie kuwa fedha hizi zitaenda kufanya kazi ili iliyokusudiwa,” alisema
Makonda
No comments:
Post a Comment