Wachezaji wa LSA wakiomba dua wakati wa michuano ya Rollingstone ilipofanyika jijini Dar.
Nahodha wa LSA, Hamdani Sarahani akimkabidhi Mhariri wa Habari wa
Tanzania Daima, Martin Malera, Kombe la LIMFA walilotwaa wakati
walipotembelea ofisi za gazeti hilo
Mkurugenzi na kocha wa LSA, Haffidh Karongo akitoa maelekezo kwa nyota
wa kikosi chake wakati wa mapumziko ya moja ya mechi za Rollingstone.
Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba kushoto akiwa katika picha ya pamoja kikosi hicho.
NA MWANDISHI WETU
MSAFARA
wa wachezaji 22 na viongozi wawili wa timu ya Lindi Soccer Academy
(LSA), umeondoka jijini Dar es Salaam leo Jumatatu asubuhi kuelekea Arusha,
kushiriki michuano ya vijana kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ya
Rollingstone (ECAYFA 2016).
LSA
yenye Makao Makuu mjini Lindi, iliondoka mjini humo jana Jumapili asubuhi na
kuwasili jijini Dar es Salaam, kabla ya leo Jumatatu kuondoka kuelekea
Arusha kushiriki ECAYFA 2016, inayoratibiwa na Akademi ya Rollingstone
ya huko.
Michuano
ya Rollingstone, ambayo inatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake na
kujijengea heshima na umaarufu, mwaka huu inatarajia kuanza kesho Juni
29 hadi Julai 9, ikishirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 13,
16 na 20.
Akizungumza
na HABARI MSETO, Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba, alisema kikosi
chake mwaka huu kitashiriki michuano hiyo levo ya vijana chini ya miaka
16, ambako nyota wake wote 22 alionao safarini wanafuzu vigezo vya
kucheza kategori hiyo.
Mkandemba
alibainsiha kuwa, kikosi kiko kamili kila idara na kwamba wana
matumaini makubwa ya kufanya vema, huku akizitaka taasisi, mashirika,
kampuni na wadau wa soka kujitokeza kuisaidia timu yake ambayo inacheza
mashindano hayo kwa mara ya pili.
Aliwataja
nyota waliomo katika msafara huo kuwa ni Hamdani Sarahani 'Mido',
Shaffih Maulid, Imani Chande, Lucas Julius, Masoud Kisige, Hassan
Alubuni, Rajabu Saidi, Mukeshi Amani, Odio Victory, Mohammed Lijei na
Banzalam Khamis.
Wengine
waliotajwa na Mkandemba kuwamo safarini ni pamoja na Madulu David, Tuwa
Saidi, Haji Mohammed, Mohammed Maneno, Ramadhani Bakari, Ramadhani
Koyo, Peter Lucas, Farouq Karongo, Shazir Issa, Faraji Nurdin na
Selemani Solomon.
No comments:
Post a Comment