Kumekuwa na taarifa za upotoshaji kuhusu uratibu na ushiriki wa klabu za Tanzania katika mashindano ya kimataifa hususani ushiriki wa Young Africans SC katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2015/2016.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limekuwa likitoa kila aina ya msaasa uliowezekana kuisaidia klabu za Young Africans na Azam ambazo ziliwakilisha nchi katika mashindanmo ya kimataifa. Kwa upande wa Young Africans awali walishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na upande wa Azam ilishiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtakumbuka, Azam FC ilitolewa na Esperance ya Tunisia katika michuano hiyo na kwa upande wa Young Africans iliposhindwa kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikashushwa na kucheza na Esperanca Sagrada ya Angola na kuitoa hivyo kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho au kwa lugha nyingine, hatua ya Makundi. TFF ikaendelea kuisaidia Young Africans kuhakikisha inashiriki vema katika mashindano hayo.
Sasa, Aprili 21, 2016 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilitoa waraka kwa timu zilizokuwa zinacheza kuwania kuingia hatua ya Makundi (Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) kupeleka majina ya maofisa watakaohudhuria warsha ya namna ya kuratibu mechi hizo kuelekea fainali. Kadhalika walitakiwa kupeleka vivuli (photocopies) vya hati zao za kusafiria.
Maofisa walihitajika ni meneja wa timu, daktari wa timu na ofisa habari wa timu. Taarifa hiyo ilikuja kabla ya Young Africans kucheza na Esperanca ya Angola. TFF iliwaataarifu Young Africans kwa kuwataka kutuma nyaraka hizo kati ya Aprili 26 na Aprili 28, 2016.
Lengo la warsha ilikuwa ni kujadili maswala ya uratibu, ufundi, udhamini na kanuni za mashindano. CAF ilijitolea kugharamia usafiri, malazi na gharama zote kwa watu watatu kutoka Young Africans SC.
Taarifa hizi na hata ukumbusho (reminders) zilipelekwa kwa baruapepe, simu na hata kuonana ana kwa ana kwa Katibu Mkuu wa Young Africans, Ofisa Habari na Viongozi wengine wa klabu.
Maofisa wa TFF kwa nyakati tofauti tofauti waliwasihi Young Africans na pia kuwakumbusha kutuma majina CAF na vivuli vya hati hati ya kusafiria, lakini kwa sababu wanazoweza kuzielezea wenyewe kwa nini hawakupeleka majina.
Mei 22, 2016 ikiwa ni siku mbili kabla ya warsha kuanza hapo Mei 24, 2016, Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bwana Baraka Deusdedit alituma majina CAF yakiwa hayana vivuli yaani photocopies vya hati ya kusafiria.
Siku moja kabla ya washiriki kuanza kuwasili Cairo, Misri, Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans alituma nyaraka kama zilivyotakiwa na wakatumiwa tiketi tatu (3) na CAF. Pamoja na tiketi kuletwa Young Africans bado watu hao hawakusafiri wakidai klabu haijatoa ruhusa.
Maofisa wa TFF wamekuwa wakifanya kazi mpaka muda wa ziada wakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka Deusdedit ili timu iweze kushiriki vema pamoja na upungufu wa kiutawala ndani ya sekretarieti yake yanayojidhihirisha wazi.
Masuala yote yanayolalamikiwa na Ofisa Habari wa Young Africans, yaliyotolewa kwa timu zote kwenye semina ya Cairo, Misri.
TFF itaendelea kuvitembelea kusaidia klabu kujenga weledi kupitia mradi wa leseni za klabu na vilevile kuratibu ushiriki wa mashindano mbalimbali.
Hata hivyo, TFF haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wa klabu wanaochafua jina la shirikisho ili kuficha madhaifu yao ya kiutawala (Administrative inefficiencies).
SHELISHELI YATUA
Timu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, imeingia Dar es Salaam, Tanzania usiku wa kuamkia leo Juni 24, 2016 saa 7.45 usiku wa kuamkia leo Ijumaa Juni 24, 2016, kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo imeingia wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na imefikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
…………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA
No comments:
Post a Comment