Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi zawadi ya Kombe la mchezaji bora Nahodha wa timu ya TASWA QUEENS, Lightness Sirikwa Mayeye, baada ya kutangazwa mchezaji bora aliyejituma katika mchezo wao dhidi ya timu ya SJAK ya Kenya.
Timu hizo zilizoshiriki katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016, zilitoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida na kupigiana penati ambapo Taswa Queens waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 4-3. Picha na
Mafoto Blog
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi Kombe la ushindi Kipa wa timu ya TASWA QUEENS, Somoe Ng'itu, baada ya timu hiyo kuifunga timu ya SJAK ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida.
Timu hizo zilishiriki kwa pamoja katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016.
Kiungo
wa timu ya Taswa Queens, Ester Zelamula
(kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, wakati wa mchezo wa kirafiki katika
Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, uliochezwa kwenye Uwanja wa
Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016. Katikati ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
Winga wa Taswa Queens, Angela Msangi (kulia) akipiga shuti huku beki wa Sjak ya Kenya, Rebecca Magoma, akijaribu kumdhibiti bila mafanikio.
Katibu wa Chama cha Waandoshi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Amir Mhando akizungumza na wachezaji wa Taswa kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
Picha ya pamoja
Kikosi cha Taswa Queens.
Muda wa mapumziko
Taswa Queens wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe chao.
Afisa kutoka Kampuni ya Bia TUSKER, Samuel Nzau, akimkabidhi Kikombe cha ushindi, Naohidha wa Sjak ya Kenya, Alex Boke baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wazee wa Taswa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Amir Mhando.













No comments:
Post a Comment