HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 16, 2016

Wenyeviti mitaa jiji la Mbeya wagoma kuendelea kusimamia shughuli za maendeleo

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

WENYEVITI wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya jijini Mbeya  wamegoma kushiriki shughuli zote za maendeleo wakiishinikiza Serikali kuwapandishia posho kutoka 20,000/  hadi 15000/ kwa mwezi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Wenyeviti wenzie wa nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa,jijini Mbeya Charles Kasyupa Mwenyekiti wa mtaa Mwafile Kata ya Ilemi alisema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo mpaka pale Halmashauri itakapo kuja na majibu ya malalamiko yao matano likiwemo la kuongezewa posho.

Kasyupa alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa wamekuwa na majumu makubwa na mengine hatarishi yakiwemo ya kusuhulishia Migogoro ya ardhi na ndoa lakini posho wanapo pewa hazilingani na kazi hiyo hiyo wanaomba Serikali iliangalia hilo kwa kuongeza kutoka kiasi haicho cha shilingi 20000/ kwa mwezi hadi shioingi 150,m000/ kwani Halmashauri imeshindwa kuwasaidia.

Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa malalamiko yao ambayo walisha opeleka katika ofisi ya Mkurugenzi lakinni mpaka sasa hayajafanyiwa kazi kuwa ni mrejesho wa fedha asilimia 20 ya mapato yatonayao ya kodi ya majengo.

Mengine ni Mikataba ya Milara ya makapuni za Simu, na Nyaya  ambazo zipo katika maeno yao Utawala,Bima ya Afya, na Vitambulisho vya kazi zao.

Akizungumza changamoto wanazo pata kutokana na kutokuwa na vitambulisho wa kazi Kasyupa alisema kuwa  wamekuwa wakipata shida sana hasa wanapoa tekeleza majukamu yao hasa wanajo jieleza kuwa wao ni viongozi wa mitaa katika vituo vya meano ya Polisi wamekuwa wakitakiwa kuitoa vitambulisho.

 ‘Tumeamua kugomea kuendelea na kazi kwani Halmashauri imeonekana kutotilia maanani malalamiko, na ukiangalia sisi wenyeviti wa Mitaa ndiyo tunaishi na wananchi na tunajua matatizo yao kuliko hawa Madiwani hivyo tunaomba Serikali iliangalie hili’ alisema Kasyupa.

Akijibu malalamiko hao Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Mussa Mapunda alisema suala la posho za mwenyeviti hao haipo katika mkataba hivyo na kwamba nafasi hiyo ni kwa ajili kujitolea na kwamba posho zinategemea zaidi mapato ya halmsahuri husika.

Aidha Mapunga alisema kuwa nafasi ya uwenyeviti wa Serikali za mitaa ni kujitolea ni hata katika fumo za kuwania nafasi hizo zinonyesha wazi.

No comments:

Post a Comment

Pages