HABARI MSETO (HEADER)


August 11, 2016

JAMANI FOUNDATION KWA KUSHIKIIAKIANA TEA YAENDELEA KUTOA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI



Mkurugenzi wa Jamani  Foundation, Nirmala Pabari (kushoto) akiwakabidhi madawati 100 Mameneja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa (kulia), na Anne Mlimuka  (wa pili kulia), kwa ajili ya shule za msingi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni mwalimu Kasyupa kutoka Shule ya Msingi Yombo ambaye aliwawakilisha waalimu wa shule zilizopokea msaada wa madawati 100.
Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania, Anne Mlimuka (kushoto),  akikabidhi madawati yaliyotolewa na  Jamani Foundation kupitia TEA  kwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja, Juto Komba katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msingi Umoja wakicheza ngoma ya asili , kutumbuiza katika hafla ya makabidhiano ya madawati.

Na Mwandishi Wetu

JAMII imetakiwa kujenga utaratibu wa kutunza vifaa vya misaada vinavyotolewa kwa ajili ya shule ili viweze kudumu na kusaidia wanafunzi kwa muda mrefu.

Ushauri Huo ulitolewa jna Meneja wa Uhamasishaji na Wateja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa wakati wakikabidhiwa madawati 100 yaliyotolewa na Jamani Foundation kwa shule za msingi Umoja na Yombo za jijini Dar es Salaam.

Alisisitiza umuhimu wa shule na wazazi kuwajengea watoto utaratibu wa kuthamini na kutunza vifaa wanavyopewa ili viweze kuduma na kunufaisha wanafinzi wengi zaidi kwa muda mrefu.

“Madawati haya 100 yamegharimu 12m/-, hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wa Jamani Foundation wanathamini mahitaji yetu nasi basi kuonyesha shukrani yetu tunapaswa kuyatunza ili yadumu na wenzetu wengine wafaidike pia na msaada huu” alisema Mganwa.

Aliishukuru Jamani Foundation kwa ushirikiano wao na Mamlaka ya Elimu katika kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuhakikisha ubora wa elimu unazingatiwa.

Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiano nayo katika kukabiliana na kero ya upungufu wa madawati na kwa sasa wanategemea kuanza ushirikiano katika mradi wa ujenzi wa vyoo ili kutunza afya za wanafunzi mashuleni.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi TEA madawati hayo, Meneja wa huduma za jamii wa Jamani Foundation, Bi Nirmala Pabari alisisitiza umuhimu wa mashirika na asasi mbalimbali kusaidia jamii ili kuboresha maisha.

Alisema wataendelea kushirikiana na serikali katika maeneo mbali mbali kulingana na mahitaji na uwezi wao lengo lao likiwa ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika mazingira bora ya upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.

Akipekea madawati hayo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Umoja, Bw Dyuto Komba alisema watatumia utaratibu wa kugawa kila dawati kwa mwanafunzi na kuandikishana na wazazi wao ili  kujenga dhana ya uwajibikaji.
“Kama tulivyofanya kwenye kugawa kitabu, na kwa madawati hivyo hivyo, yatapewa namba na majina ambapo kila mwanafunzi atapaswa kulitunza na likiharibika mzazi au mlezi atawajibika kwa matengenezo” alisema.
Alisema baada ya msaada huo, shule yake haina tena shida ya madawati na kusema changamoto waliyonayo ni uhaba wa madarasa hasa kutokana na kuongezeka kwa usajili wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi.

No comments:

Post a Comment

Pages