Mchezaji Veronica
Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo
wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro
Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 (Picha na Selemani, Semunyu)
Na Selemani Semunyu, JWTZ
Timu ya
Mpira wa Pete Netball ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ime3rejesha
heshima yake baada ya Kuwafunga mabingwa Watezi
wa Michuano hiyo kwa Mpira wa Pete Uganda kwa magoli 29 kwa 27.
Katika
Mchezo huo uliokuwa wa Vuta nikuvute na
rabsha za hapa na pale zilizizojitokeza kabla wakati na Baada ya Mchezo huo
ambao ulikuwa na Upinzani Mkali kutokana na historia ya Timu hizo.
Katika Robo
ya Kwanza Tanzania ilimaliza ikiongoza kwa magoli saba kwa Sita huku Timu zote zikicheza
Mchezo wa kuviziana lakini uliojaa nguvu na kukamiana miongoni mwa Wachezaji.
Katika Robo
ya Pili Tanzania pia ilimalizai ikiwa mbele kwa mabao 13 kwa 11 kukiwa na
tofauti ya magoli mawili tofauti na robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa
tofauti ya goli moja.
Robo ya Tatu
Uganda walikuja na kusawazisha na kasha kuongeza na hivyo kumaliza kwa ushindi
wa magoli 20 kwa 19 ya Tanzania na
kuwafanya Tanzania kwenda kujiuliza.
Hatimaye
robo ya Mwisho ikamalizika na Timu ya Tanzania kuibuka na Ushindi na hivyo
kuwatisha Mabingwa wa mwaka uliopita pengine utarejea kwa Tanzania
Kwa Upande wa Nahodha wa Timu hiyo Dorita
Mbunda alisema mechi yao na Uganda wamecheza kama fainali kutoka na historian a
kuahidi kujipanga kwa ajili ya kuwakabili Kenya.
Kwa upande
wake Nahodha Uganda Lilian Ajio amelalalimika Waamuzi kutoelewa Sheria Mpya za
Mchezo huo hali iliyopelekea wakati mwingine kutokuwa na maamuzi sahihi.
No comments:
Post a Comment