NA FRANCIS DANDE
WANANCHI wa mtaa wa Mwembeni Kata ya Manzese jijini Dar es
Salaam wameibua taharuki baada ya kwenda kutupa uchafu ‘Taka taka’ kwenye Ofisi
ya Serikali ya Mtaa wa Mwembeni.
Uamuzi ulitokana na madai ya wananchi hao kwamba ofisi
hiyo imeshindwa kutekeleza utaratibu wa kuzoa taka kwenye maeneo hayo takribani
kwa miezi mitatu.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
baadhi ya wananchi hao walibainisha kuwa wamekuwa wakitozwa ushuru wa kuzolewa
uchafu kila mara lakini hakuna gari lililokuwa likizo taka hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi hapo, Ofisa
Mtendaji wa Kata hiyo, Fatuma Abdallah ambaye akutaka kupigwa picha alikiri
kwamba ni kweli tatizo la kuchukua taka limekuwa sugu mtaani hapo.
Alisema hapendi kuona uchafu ukikithiri hadi kufikia hatua
ya wananchi kumfikishia taka ofisi kwake lakini imewaradhimu kutokana na mfumo
uliopita ulikuwa mbovu katika usimamizi.
“Mimi ni mgeni hapa, nina miezi mitatu tangu nianze kazi
na nimekuta kuna deni la ubebaji taka jambo ambalo limenipa wakati mgumu katika
kusimamia uzoa wa uchafu kwa muda muhafaka,” alisema.
Mjumbe wa Shina namba 57, Zainab Abdalah amesema kuwa
kutokana na kero ya uchafu uliorundikana majumbani kwao wameamua kuja kuzileta
katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa ili kuushinikiza uongozi wa Kata hiyo
kuziondoa taka hizo zilizorundikana majumbani kwao.
Naye Mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Odo
Said alisema kuwa wamekuwa wakichangishwa kiasi cha shilingi 2000 kwa mwezi kwa
ajili ya kupata huduma ya kuzolewa taka lakini hata wanapofanya hivo magari
yamekuwa hayafiki kwa wakati na kusababisha mrundikano wa taka nyingi majumbani
na hivyo kuhatarisha afya zao kutokana na kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko
kama kipindupindu.
Lundo la uchafu likiwa limetupwa nna wananchi wa Mtaa wa Mwembeni nje ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwembeni, Manzese jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua ya kuushinikiza uongozi wa Kata hiyo kuzoa taka zilizolundikana katika makazi yao.
Mkazi wa Mtaa wa Mwembeni akitupa taka nje ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwembeni Kata ya Manzese.
Mkazi wa Mtaa wa Mwembeni Manzese jijini Dar es Salaam akitupa taka nje ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa baada ya gari la kuzoa taka katika mtaa huo kushindwa kupoita kwa wakati na kusababisha mlundikano wa taka majumbani.
Mkazi wa Mtaa wa Mwembeni
Manzese jijini Dar es Salaam, Rajabu Kassim akitupa taka nje ya Ofisi ya Serikali ya
Mtaa baada ya gari la kuzoa taka katika mtaa huo kushindwa kupoita kwa
wakati na kusababisha mlundikano wa taka majumbani.
Wananchi wakiingia katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwembeni jijini Dar es Salaam kupata huduma huku lundo la uchafu likiwa mlangoni.
Taka zikitupwa nje ya Ofisi za Serikali ya Mtaa na kusababisha ofisi nzima kutoa harufu kali.
No comments:
Post a Comment