Na Talib Ussi na Maua Muhammed, Zanzibar
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), limemfukuza uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba kwa madai ya kukiuka madili ya chama hicho ikiwemo kuongoza kikundi cha wahuni na kuhujumu mali za chama hicho.
Akizungumza na wandishi wa habari huko ofisi ya chama hicho ilioko Vuga mjini Zanzibar Mwenyekiti wa kikao hicho Katani Mohamed katani alisema baraaza kuu limechukua mamuzi hayo bada ya kujiridhisha na taarifa zote.
“Baraaza kuu linaaweka bayana kwa wanachama wa CUF watanzania na mamlaka zote nchini kuanzia Septemba 27 profesa Ibrahim Lipumba hana haki ya kujihusisha na namna yeyote ile na shughuli za chama”alisema katani.
Kwa mujibu wa Katani Baraza kuu la uongozi limeridhika kwamba kamati ya utendaji ya taifa ilimfikishia profesa Lipumba barua ya wito yenye kumbu kumbu namba CUF/HQ/OKM/WM/2016/VOL.1/49 ya tarehe 24/09/2016 ambapo pia ilikuwa na maelezo ya tuhuma na kumtaka afike mbele ya kikao hicho cha leo.
“Lengo la wito huo ni kuja kujieleza mbele ya kikao cha baraza kuu kuja kujieleza na kujitetea kwa nini asichukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa katiba ya chama cha CUF kwa kuvunja masharti yanayohusu wajibu wa mwananchama” alieleza Katani.
Kikao cha baraza kuu kiliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 80 (1). Ambapo Wajumbe 43 kati ya wajumbe 53 wa Baraza
Walihudhuria kikao hicho walipo sasa.
Ambapo alieleza kuwa ili baraza hilo lifikie kutoa maamuzi lazima wajumbe wafikiao nusu waweza kuhudhuria lakini alisema kikao hicho wamefika wajumbe 43 kati ya 53 wa sasa.
Alieleza kuwa Agenda za kikao hicho zilikuwa ni tatu zilizotayarishwa na kuwasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa zilijadiliwa na kufanyiwa maamuzi ambazo ni pamoja na Kujadili barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya tarehe 23/09/2016;
Kupokea na kujadili mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kutokana na hujuma alizozifanya tarehe 24/09/2016 Afisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam na Kumjadili na Kumhoji Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya kikao na kumchukulia hatua za kinidhamu.
Baada ya mjadala wa kina wa agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio na maamuzi ikiwemo kuukata ushauri ushauri, msimamo na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya Siasa alioutoa kupitia barua yake ya tarehe 23/09/2016.
Alisema Baraza limelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana dharau alioionesha Pr Lipumba kwa kupokea wito na kushindwa kuhudhuria katika kikao hicho ili kuji tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
“ kwa sababu Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) – Sura ya 258 haimpi mamlaka wala uwezo wowote kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama na kwa kulitambua hilo ndiyo maana katika matamko yake yote aliyoyatoa,ameshindwa kutaja kifungu gani cha sheria kinampa uwezo huo” alieleza Katani.
Aidha alifahamisha kuwa Baraza Kuu limesikitishwa sana na kitendo cha Jaji Francis Mutungi kujishushia hadhi, kujifedhehesha na kujivunjia heshima mbele ya macho ya jamii ndani na nje ya nchi, yeye na Ofisi anayoiongoza kwa kuvunja sheria na kudharau maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of 2003) ambapo Jaji Mihayo aliamua kwamba:
“… Sioni popote katika Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo Msajili ana madaraka ya kubariki au kupinga vikao vya vyama vya siasa ay maamuzi ambayo vikao hivyo vinafanya.”
Sambamba na hilo Baraza Kuu limemuagiza Katibu Mkuu wa Chama kumjibu kwa maandishi na kwa kina Msajili wa Vyama vya Siasa na kumueleza maamuzi ya Baraza hilo ambalo kikatiba ndilo lenye madaraka ya kusimamia uendeshaji wa Chama kwamba halitambui ushauri, msimamo na mwongozo huo na limeutupilia mbali kwa kukosa kwake mantiki, hoja na pia kukosa nguvu za kisheria.
Aidha Baraza Kuu hilo linamtanabahisha Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba atabeba dhamana kwa yote yaliyofanywa na yatakayofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake cha wahuni ambacho kilivamia Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 na kupiga watu na kufanya uharibifu wa mali kutokana na tamko lake hilo ambalo halina msingi wa kisheria.
Katika hatua nyengine +Baraza Kuu limepokea mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba yaliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 80 (1) ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia nidhamu ya Chama katika ngazi ya Taifa na kuyawasilisha mapendekezo yake mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
Alieleza kuwa Baraza Kuu limeridhika kwamba Kamati ya Utendaji ya Taifa imefuata masharti yote ya Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014) katika kuanda mashtaka hayo kutokana na mtuhumiwa, Prof. Ibrahim Lipumba, kuvunja Katiba ya Chama, Ibara ya 12 inayohusu ‘Wajibu wa Mwanachama” hasa Ibara ndogo za 12 (6), 12(7) na 12(16).
Kwa upande mwengine Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho AbuuBakar Khamis Bakar alieleza kuwa Baraza Kuu ni chombo Pekee ambacho kinaweza kumchukulia mtu hatua na si mtu mmoja mmoja kama kifungu cha 80 cha katika ya CUF toleo la 2014.
No comments:
Post a Comment