HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2016

CDF TROPHY YAANZA KWA KASI LUGALO GOLF CLUB

Mwenyekiti wa Klabu ya golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo (Katikati) akiangalia mazoezi ya wachezaji wa Klabu hiyo wanaotaraji kushuka Uwanjani kuwania  CDF Trophy ( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akikata utepe kuzindua Daraja la Kiwanja namba Tisa cha  Golf Lugalo ikiwa ni sehemu ya kuboresha uwanja huo na kuwa na sifa zaidi kwa mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa.

SelemaniSemunyu, JWTZ

Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf CDF Troph imeanza kwa Michezo ya awali ambapo  Wapiga mikwaju wa kulipwa wamechuana vikali huku Geofrey Reverian  na Klabu Lugalo na Farai Chitengwa  wa Zimbambwe wakilazimika kurudia mchezo baada ya kufungana.

Katika mashindano hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Lugalo Golf Club Jijini Dar es salaam wamefungana mikwaju ya jumla (gross) 72 kwa kila mmoja na kulazimika kutakiwa kurudia mchezo kwa kucheza viwanja vitatu hali itakayoamua nani kuibuka mshindi katika kundi la wapiga mikwaju wa kulipwa.

Katika nafasi ya tatu ya Wapiga Mikwaju hao wa  kulipwa imechukuliwa na Salim Mwenyenza aliepata mikwaju ya Jumla 74 ikiwa ni kati ya wachezaji wa kulipwa 20 walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ambacho mshindi atajulikana jumamosi Septemba 23 mwaka huu.

Katika hatua Nyingine wacheza Golf wa kundi la Wachezaji Wasaidizi (Carde) 30 walipambana kupata mbabe wa kundi hilo ambapo Richard Mtweve aliibuka na ushindi kwa kupata Net 69 baada kupigaMikwaju ya Jumla 76 huku akicheza kwa kiwango cha Saba.

Nafasi ya  pili imechukuliwa na Rasuri Shaban baada ya kupata Net 70 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 79 huku kiwango cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na Mwanamke pekee kwa kundi hilo Rose Nyenza kushika Nafasi ya tatu baada ya kupata net ya 87 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 111 na kiwango cha Uchezaji kikiwa ni 24.

Michezo hiyo ya Kombe la Mkuu wa  majeshi ya Ulinzi CDF Trophy yanatarajiwa kuendelea na kufikia tamati Jumamosi Septemba 24 katika Uwanja wa Golf wa Lugalo ambapo wachezi wa makundi matatu watachuana.

Makundi hayo ni Senior,Junior, Ladies na  Daraja la A Daraja B na daraja C  ambapo mbapo pia mshindi wa Jumla atapatikana kutoka katika Makundi hayo.
Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo ya Kombe la Mkuu wa majeshi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Pages