NA KENNETH NGELESI,RUNGWE
SHULE ya Sekondari ya Kisondela iliyopo Kata ya Kisondela Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya haina walimu wa masomo ya Sayansi kwa zaidi ya miaka kumi na Mbili hali inayosababisha wanafunzi kupata matokeo mabaya katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo, Yusuf Mwakyambiki mwanafunzi wa darasa la nne alisema kuwa hawana walimu wa masomo ya fizikia na baiologia tangu mwaka 2004 hadi sasa lakini hulazimishwa kufanya mitihani ya kitaifa katika masomo hayo.
‘Walimu tuano wachache tuna moja wa Kemia hivyo kutoka kidato cha kwanza tumekuwa tukikongoja kwa kutafauta walimu ambao shule ilikuwa inawalipa kwa kutumia fedha za michango likini baada ya kuja sera ya kutolewa elimu bure hatuna mwalimu kwani hakuna cha kuwalipa nma wazazi hawaelewi hivyo ni vema Serikali ikilifafnua hili’ alisema Mwakyambiki
Kutokana na uhaba wa walimu hao, wameitaka serikali kufanya jitihada za haraka kupeleka walimu wa masomo ya Sayansi ili kuwaondolea kero hiyo.
Mkuu wa shule hiyo Dick Mwaikambo alisema tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya Sayansi linachangiwa na wanafunzi wenyewe kudaiwa kufanya vibaya katika mitihami ya masomo hayo huku ukiiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hiyo iliyodumu kwa muda wa miaka kumi na mbili hadi sasa.
Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa Kata hiyo Julietha Senga alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba tayari kata ilisha peleka changamoto hiyo halmashauri ili kuzishughulikia huku akiwataka wanafunzi kuwa na subira.
Hata hivyo, Afisa Elimu wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mussa Shabani Ally amesema uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni tatizo la nchi nzima ambalo serikali ipo katika hatua za kulitatua.
No comments:
Post a Comment